Lil Wayne anaendelea na maisha yake akiwa jela katika kisiwa cha Rikers na hivi sasa bosi huyo wa Young Money amepatiwa kazi maalum ya kufanya akiwa jela. Antonia Toya ambaye ni mpenzi wa lil wayne tangu wakisoma pamoja sekondari na pia mama wa binti wa Wayne aliye na miaka 11 sasa Reginae Carter amesema kazi ya Wayne jela ni kuangalia wafungwa wenzake wasiuane anawaangalia wafungwa walioshindikana wasipigane hadi kuuana, inaonyesha jamaa ni mtemi kuwazuia watemi, wababe kuacha kugombana ni kazi kubwa sana lakini anaipenda kazi hiyo ambayo haimlipi Nyota huyo wa Hip hop anatumikia jela mwaka mzima kutokana na kosa la kumiliki silaha kinyume cha sheria baada ya kuhukumiwa mwezi uliopita lakini jela za wenzetu ni nzuri kwani hadi hivi sasa hajakata nywele zake ndefu