Posts

NEW YEAR MYSTERY AT MALAIKA BEACH

Image

HAWA NDIO BAADHI YA WASANII WALIOFANYA SHOW NYINGI KWA KIPINDI HIKI CHOTE CHA MWAKA 2011.

Image
Ally Kiba ni msanii aliyefanya vizuri sana kwa mwaka huu 2011 kwa kutoa wimbo wake uliobeba jina la Dushedede. Wimbo huu umempa show kibao za ndani na nje ya nchi na kujikuta anafunga mwana vizuri na kuweka kumbukumbu kwa kufanya show nyingi na kuendelea kuongeza idadi ya mashabiki kote duniani. Dully Sykes aka Brazamen aka Mr. Misifa, huyu bwana kwa mwaka huu ametoa wimbo uliobeba jina la Bongo Fleva nakupa show nyingi hapa bongo na nje ya mipaka ya bongo. Dully ni msanii ambaye kwa mwaka huu amepiga show nyingi hadi kufikia kuwa kwenye tangazo ya kampuni moja ya simu hapa nchini.   Linah msanii bora wa kike kwa mwaka huu aliyefanya vizuri kwa kuchukua tuzo mbili za Kili Music Award, moja ikiwa kama Mwimbaji bora wa Kike na ya pili ni kama msanii bora anayechipukia. Pia kwa mwana huu Linah ameweza kwenda New York kwenye tuzo za mama Laura Bush na Atlanta   kwenye mkutano wa Ushers New Look Foundation . Linah kwa mwaka huu amepiga show ny...

NAWATAKIA MAANDALIZI MEMA YA MWAKA MPYA 2012

Image

NDANI YA VICTORIA FM 90.6 MHz

Image
Nikaachiwa mtambo kidogo hapa ni kapata chance ya kukutana na mwanadada Khadija Hassan ambaye ni mtangazaji wa kipindi cha Extravaganza show..flash ikatumulika.      

MAPACHA 3, WAPAGAWISHA GOLD CREST, MWANZA

Image
Kalala Junior Khalid Chokoraa Mama yake Kalala Junior naye alikuwepo Jose Mara Benard James wa Star TV, Hakupitwa Dancer No 1 wa Mapacha 3 Dancer No 2 wa Mapacha 3 Dancer No 3 wa Mapacha 3 Mhariri wa Star TV Moses, akiwa na ndugu zake naye alikuwepo Mpiga solo mahiri wa Mapacha 3 Mpiga Rythm mahiri wa Mapacha 3 Mpiga Bass Gitaa mahiri wa mapacha 3 Mpiga Tumba mahiri wa mapacha 3 Mpiga Bass Gitaa mahiri wa Mapacha 3 Kundi zima la mapacha 3 Mashibiki hawakujivunga kusakata nyimbo za mapacha 3 ndani ya Gold Crest Mwanza Madansa wa Mapacha 3 wakikaribisha mashabiki wao kwenye moja ya nyimbo za Mapacha 3 Mapacha 3 wakishambulia jukwaa Shabiki No 1 wa Mapacha 3, Jose!!                                    Picha na habari ni kutoka  www.thebigtopten.blogspot.com

MAFURIKO YA DAR..............

UTATA mkubwa umegubika idadi halisi ya watu waliopoteza maisha kwenye mafuriko yaliyotokea jijini Dar es Salaam. Wakati serikali ya mkoa ikisisitiza kuwa idadi ya waliopoteza maisha ni 38, zipo taarifa kuwa idadi hiyo inafichwa na serikali kwa sababu isizopenda kuzitaja. Akizungumzia kuhusu suala hilo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadik, alisema idadi ya watu waliokufa mpaka jana kwa mujibu wa takwimu za serikali ni watu 38. Alisema kama kuna watu wanazo taarifa zaidi juu ya vifo vilivyosababishwa na mafuriko wazipeleke sehemu zinazohusika. “Hatuna sababu ya kuficha vifo vya watu, sisi tunatangaza idadi ya maiti tulizoziona si vinginevyo,” alisema. Aliongeza kuwa ni jukumu la kila mmoja kushirikiana na serikali kuwahudumia waathirika wa mafuriko hayo ambao mpaka sasa wamefikia 5,000. Wakati utata ukigubika juu ya maiti hizo, baadhi ya wananchi wa maeneo ya Jangwani wamelidokeza Tanzania Daima Jumapili, kuwa wameanza kusikia harufu za kuoza kwa vitu, na wameweka bayana kuw...

CPWA ROCKS HHHHMMM...OFFICIAL VIDEO

Image