TAARIFA KUTOKA TCU KUHUSU UDAHILI KWA MWAKA WA MASOMO 2012/2013
UTANGULIZI Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (‘ Tanzania Commission for Universities ’ -TCU ) ikishirikiana na Baraza laTaifa la Elimu ya Ufundi (‘ National Council for Technical Education’ - NACTE ) pamoja na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi Elimu ya Juu ( Higher Education Students Loans Board ) inapenda kuutarifu umma kuhusu utaratibu wa kujiunga na vyuo vya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2012/2013 kupitia mifumo ya “Pre-entry”, “Mature Age Entry”, “Equivalent Qualifications” na mfumo wa pamoja wa udahili (‘Central Admission System’) na utaratibu wa mikopo kama ifuatavyo: 1. MFUMO WA UDAHILI KUANZIA MWAKA 2012/13 1.1 Utaratibu wa Kuendesha Program za “Pre-entry” na “Mature Age Entry” Kuanzia mwaka huu 2012, vyuo vyote vitakavyotaka kuendesha mafunzo ya awali kabla ya mwombaji kustahili kudahiliwa ili kuweza kujiunga na programu za elimu ya juu (pre-entry programmes) pamoja na kuendesha mitihani ya kupitia mfumo wa “Mature Age Entry” vinataki...