MPIGIE KURA MALFRED ALFRED

UJUMBE WA KUTOKA KWA RAFIKI YANGU MALFRED ANAOMBA MPENZI WA BLOG HII UMPIGIE KURA KATIKA KILIMANJARO MUSIC AWARDS
Napenda kuwafahamisha marafiki wangu wote na mashabiki wangu kuwa baada ya kuchaguliwa kuingia katika kinyang'anyiro cha kumtafuta mwanamuziki bora wa Reggae na Ragga katika Tuzo za Kilimanjaro Music Awards kwa mwaka huu 2012 nilifanikiwa kuingia na nyimbo tatu,

Katika Category ya RAGGA/DANCEHALL nina nyimbo mbili POYOYO na KUDADADEKI,

Na katika Category ya REGGAE nina wimbo MAZINGIRA FT LUTAN FYAH,

Ni wakati wangu wakukuomba kura yako kwa hali na mali ukiwa kama Ndugu,Rafiki,Shabiki,na hata adui pia kwani kura yako itaniwezesha kushinda.

Ili kuzipigia kura nyimbo zangu KATIKA CATEGORY YA RAGGA/DANCEHAL nenda sehemu ya kuandikia sms katika cm yako andika "M4"kisha tuma kwenda 15747 hapa utakuwa umeipigia kura "KUDADADEKI" na ukiandika "M5"kwenda 15747 hapa utakuwa umeipigia "POYOYO" pia kuna njia nyingine rahisi kwa wale wa Internet pia nenda sehemu yakundika email andika 'M4'wimbo ni "KUDADADEKI" kwenda,[ktma@innovexdc.com] "M5"ni wimbo"POYOYO"kisha tuma hivyo hivyo,

Kunipigia KURA katika CATEGORY YA REGGAE wimbo"MAZINGIRA ft LUTAN FYAH"andika K1 sehemu ya kuandikia sms katika cm yako kisha tuma kwenda 15747,Au kwakutumia email nenda sehemu yakuandikia ujumbe andika K1 kisha tuma kwenda [ktma@innovexdc.com]kumbuka unaruhusiwa kuupigia wimbo mmoja kura moja,ila mtu mmoja anaweza kuzipigia kura nyimbo zote tatu kwa wakati mmoja,ukishapiga hurusiwi kuzipigia tena,pia waweza kunipigia kura katika tovuti hizi,[www.kilitimetz.com]au [www.teentz.com]

Ninaomba sana kura yako na ninakushukuru kwakusoma maelezo haya marefu
Shukrani sana,One love

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA