Posts

Mgonjwa wa Ebola agundulika Newyork

Image
Mji wa Newyork Daktari wa Marekani aliyekuwa akiwahudumia wagonjwa wa Ebola Nchini Guinea amepimwa na kukutwa na virusi vya ugonjwa huko katika hospitali ya ya mjini Newyork. Dr Craig Spencer ambaye ni mmoja kati ya madaktari wasio na mipaka alianza kujisikia maumivu na homa siku chache tu baada ya kurejea Marekani akitokea Afrika Magharibi. Siku ya Alhamisi wiki hii Craig alipelekwa hospitali kwaajili ya vipimo na kisha akatengwa kwa uchunguzi zaidi wa afya yake. Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Meya wa mji wa Newyork Bill de Blasio amesema watu hawapaswi kuwa na hofu kwani hatua zote mhimu zilifuatwa katika kumchunguza Dr.Craig na hadi alipobainika kuwa na maambukizi hayo. Kubainika kuwa na virusi vya ugonjwa wa Ebola kwa Dr.Craig kunaongeza idadi ya waliobainika kuwa na ugonjwa huo nchini Marekani kutoka watatu na kufikia wagonjwa wanne. Chanzo:BBC

MAGAZETI YA LEO IJUMAA, OCTOBA 24

Image
\

Picha za mazoezi ya pamoja ya Wanajeshi wa Tanzania na China

Image
Askari wa majini wa Tanzania na China, wakiwasubiri maelekezo mwanzoni mwa mazoezi ya pamoja ya kijeshi kwenye komandi kuu ya wanamaji wa JWTZ, Kigamboni jijini Dar es Salaam, Jumanne Oktoba 21, 2014. Mkuu wa Operesheni na Mafunzo wa JWTZ, Meje Jenerali James Mwakibolwa, (Kulia) na Meja Jenerali Wu Xiao Yi wa jeshi la wanamaji la China, wakibadilishana hati za makubaliano ya mafunzo ya pamoja ya Surpassing 2014. Mwanajeshi wa kikosi maalum cha wanamaji kuitoka jeshi la China, akionyesha matumizi ya mikono dhidi ya adui, wakati wa uzinduzi wa mazoezi ya kijeshi ya pamoja kati ya Wanamaji wa China na Tanzania kwenye kamandi kuu ya kikosi cha wanamaji, Kigamboni jijini Dar es Salaam, Jumanne Oktoba 21, 2014. Mazoezi hayo yaliyopewa jina "Surpassing 2014" yalianza kwa maonyesho ya matumizi ya mikono katika kupambana na adui pamoja na maonyesho ya zana za kivita ambapo Mkuu wa Operesheni na mafunzo wa JWTZ, M...