Mgonjwa wa Ebola agundulika Newyork

Mji wa Newyork
Daktari wa Marekani aliyekuwa akiwahudumia wagonjwa wa Ebola Nchini Guinea amepimwa na kukutwa na virusi vya ugonjwa huko katika hospitali ya ya mjini Newyork.

Dr Craig Spencer ambaye ni mmoja kati ya madaktari wasio na mipaka alianza kujisikia maumivu na homa siku chache tu baada ya kurejea Marekani akitokea Afrika Magharibi.

Siku ya Alhamisi wiki hii Craig alipelekwa hospitali kwaajili ya vipimo na kisha akatengwa kwa uchunguzi zaidi wa afya yake.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Meya wa mji wa Newyork Bill de Blasio amesema watu hawapaswi kuwa na hofu kwani hatua zote mhimu zilifuatwa katika kumchunguza Dr.Craig na hadi alipobainika kuwa na maambukizi hayo.

Kubainika kuwa na virusi vya ugonjwa wa Ebola kwa Dr.Craig kunaongeza idadi ya waliobainika kuwa na ugonjwa huo nchini Marekani kutoka watatu na kufikia wagonjwa wanne.

Chanzo:BBC

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA