Posts

YANGA VS AZAM NGOMA DROO, WATOKA SARE YA 2-2

Image
Mshambuliaji wa Yanga, Danny Mrwanda (kulia) akijaribu kumtoka beki wa Azam FC. Kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima akiwa kazini wakati wa mechi ya leo dhidi ya Azam FC. TIMU za Yanga na Azam FC leo zimeshindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya bao 2-2 kwenye mtanange wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Mabao ya Azam yamewekwa kimiani na Didier Kavumbagu katika dakika ya 5… Mshambuliaji wa Yanga, Danny Mrwanda (kulia) akijaribu kumtoka beki wa Azam FC. Kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima akiwa kazini wakati wa mechi ya leo dhidi ya Azam FC. TIMU za Yanga na Azam FC leo zimeshindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya bao 2-2 kwenye mtanange wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Mabao ya Azam yame...

NDEGE NYINGINE TENA YAPOTEA NI AIR ASIA

Image
  Bado dunia imebaki njia panda juu ya wapi ilipo ndege ya Malaysia Airlines 370 ambayo ilikuwa na abiria 239, ilipotea miezi zaidi ya nane iliyopita ikitokea Malaysia kwenda China, ndege nyingine imepotea, ilitokea Singapore kwenda Indonesia. Iliyopotea saa chache zilizopita ni AirAsia qz 8501,  ilikuwa na abiria 162 wengi wao walikuwa raia wa Indonesia na Uingereza imethibitisha kuwa kuna mtu mmoja raia wa nchi hiyo alikuwa akisafiri na mtoto wake. Ndege ilipotea wakati rubani alipolazimika kubadili mwelekeo wa ndege hiyo pasipo kuomba mwelekeo kutoka kwa waongozaji kutokana na hali mbaya ya hewa. Ndugu, jamaa na marafiki wa watu waliokuwa wakisafiri kwa ndege hiyo wamejikusanya katika uwanja wa ndege wa Surabaya Indonesia , wakisubiri kupata taarifa yoyote itakayokuwa na matumaini kwao. Baadhi ya vikosi vinavyotafuta ndege hiyo vimesitisha zoezi hilo kutokana na hali mbaya ya hewa huku vingine vikiendelea.

50 CENT ACHUKIZWA NA TABIA YA ONGEZEKO LA MAUAJI YA WATU WEUSI MAREKANI

Image
Mwaka hauishi vizuri kwa Raia wa Marekani ambao wana asili ya Afrika, ile story ya ubaguzi ambayo huenda Dunia ilidhani imekwisha imechukua sura mpya kila kunapokucha, kinachosababisha story kuwa kubwa zaidi ni kitendo cha hali hiyo kujitokeza ndani ya Taifa la Marekani. Tumeona Marekani ikiwa mstari wa mbele kupambana na vingi, hii ishu ya ubaguzi wa rangi ni changamoto kubwa taifa hilo kwa sasa. Wameuawa wengi tayari ndani ya kipindi kifupi, watu hao wenye asili ya Afrika wameandamana na kutumia njia mbalimbali kuonyesha hawakuridhishwa na Mahakama kuwaachia huru Askari ambao wamefanya mauaji hayo. Kutokana na matukio hayo ya mauaji kuendelea kujitokeza rapper  50 Cent , ameamua kuvunja ukimya na kujitokeza kuelezea kukasirishwa kwake na matukio hayo ya mauaji na kupost picha ya  Hayati  Mahatma Gandhi  iliyoandikwa “ An eye for an eye makes the whole world blind “. Kisha akaandika ujumbe wa kuwafariji waliopata athari kutokana na tukio hilo;...

Idris Elba Ajibu Mashambulizi Ya Waliomponda Sababu Ya Rangi Yake baada ya kutengeneza movie na kuigiza kama James Bond

Image
Staa wa filamu ya The ‘Mandela: Long  Walk to Freedom   Idris Elba ametoa mtazamo wake kuhusu uvumi kuwa anatarajiwa kuchaguliwa kuigiza kama James Bond kwenye filamu za 007  zijazo. Kilichopeleka Idris kutoa mtazamo wake ni maneno mabaya ya ubaguzi yaliyotolewa na baaddhi ya mashabiki wa filamu hio kutoka Uingereza waliosema Idris ni mweusi ha wawezi kuwa James Bond kwa  sababu ya rangi yake. Kupitia twitter Idris ameandika “ Isn’t 007 supposed to handsome? Glad you think I’ve got a shot! Happy New year people, ” Twit ya Idris inamaana ”  Si 007 anatakiwa awe na mvuto ? nashukuru mnaodhani natakiwa kupata nafasi hii, heri ya mwaka mpya watu “ Limbaugh amesema  husika ya James Bond ilitengenezwa na  Ian Fleming kachero aliyefanya kazi  MI6 ya Uingereza na James Bond alikuwa mweupe na Mscottish . Aliendelea kusema  tumekuwa na James Bond weupe kwa miaka 50 sasa , nilazima awe Mscottish na awe anakunywa vodka iliyotingishwa na sio ...

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI, DECEMBER 28 YAPO HAPA

Image
. . . . . . . . . . . . . . . . .

GOOD NEWS: VANESSA MDEE ASHINDA TUZO NCHINI NIGERIA YA BEST FEMALE EAST AFRICA

Image
Kupitia ukurasa wake wa instagram, msanii wa muziki wa kizazi kipya na mtangazaji wa kituo cha Choice Fm,Vanessa Mdee aka V-Money kaandika "To God be the glory, Thank you soo much for voting. I love you"#BestFemaleEastAfrica #Tanzania amewashukuru mashabiki wake kuashiria ushindi huo alioupata katika kipengele cha Best Female EastAfrica nchini Nigeria kupitia tuzo za AFRIMA

NEW VIDEO: BONGE MOJA LA KICHUPA "SHAKE SHAKE" YA MSAMI

Image
Naileta kwenu video mpya ya Msanii Msami inaitwa Shake Shake na imetayarishwa na kuongozwa na Aby Kaz