50 CENT ACHUKIZWA NA TABIA YA ONGEZEKO LA MAUAJI YA WATU WEUSI MAREKANI
- Get link
- X
- Other Apps
Mwaka hauishi vizuri kwa Raia wa Marekani ambao wana asili ya Afrika, ile story ya ubaguzi ambayo huenda Dunia ilidhani imekwisha imechukua sura mpya kila kunapokucha, kinachosababisha story kuwa kubwa zaidi ni kitendo cha hali hiyo kujitokeza ndani ya Taifa la Marekani.
Tumeona Marekani ikiwa mstari wa mbele kupambana na vingi, hii ishu ya ubaguzi wa rangi ni changamoto kubwa taifa hilo kwa sasa.
Wameuawa wengi tayari ndani ya kipindi kifupi, watu hao wenye asili ya Afrika wameandamana na kutumia njia mbalimbali kuonyesha hawakuridhishwa na Mahakama kuwaachia huru Askari ambao wamefanya mauaji hayo.
Kutokana na matukio hayo ya mauaji kuendelea kujitokeza rapper 50 Cent, ameamua kuvunja ukimya na kujitokeza kuelezea kukasirishwa kwake na matukio hayo ya mauaji na kupost picha ya Hayati Mahatma Gandhi iliyoandikwa “An eye for an eye makes the whole world blind“.
Kisha akaandika ujumbe wa kuwafariji waliopata athari kutokana na tukio hilo; “Condolences to the family of the 2 officers.RIP Mike Brown, RIP Eric Garner randomly shooting police officers is not the answer. Mayor De Blasio get your ass to work!!!! #SMSAUDIO #POWERTV #FRIGO#EFFENvodka”– @50cent
Sorce:millard ayo
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment