KADA ACHUKUA FOMU, ATEMBEA HADI STENDI
Kada wa CCM, Antony Chalamila (mbele kulia) akitembea kwa miguu wakati ekienda kutafuta basi la kumrejesha mkoani Morogoro, baada ya kuchukuwa fomu za kuomba kugombea kiti cha Urais kupitia chama hicho, mjini Dodoma jana. Picha na Edwin Mjwahuzi. Antony Chalamila (66) amekuwa mgombe wa 41 kuchukua fomu ya kuomba kupitishwa na CCM kuwania urais, lakini kivutio kilikuwa ni jinsi alivyochapa mguu kutoka ofisi za chama hicho hadi stendi ya mabasi kurudi mkoani Morogoro. Wakati kada huyo akijitokeza tano kabla ya muda wa kuchukua na kurejesha fomu kuisha, makada wengine wawili walirejesha fomu, huku Balozi Amina Salum Ali akilalamikia kukithiri kwa rushwa katika mchakato. Chalamila, ambaye aliongozana na msaidizi wake Benjamin Ruvunduka kwenda kuchukua fomu ofisi za makao makuu ya CCM, hakuwa na usafiri wowote wakati wa kuondoka na hivyo kutembea umbali wa takriban kilomita 1.2 kwenda kituo cha mabasi kurejea mkoani kwake Morogoro. (P.T) “Naelekea Morogoro hivi sasa wananisub...