NE-YO KUFANYA MAKAMUZI KWENYE TUZO AMBAZO DIAMOND NA VANESSA MDEE WANAWANIA!

Ne-yo.
STAA kutoka nchini Marekani ambaye ni mwimbaji, mwandishi wa mashahiri, dansa na mwigizaji, Ne-yo ni mmoja mwa wasanii watakaotoa burudani katika utoaji Tuzo za Muziki za MTV Africa (MAMAs) huko nchini Afrika Kusini.

Taaarifa hiyo imethibitishwa na habari iliyowekwa katika akaunti ya Twitter ya MTV Africa ikieleza kuwa mkali huyo wa R&B tayari amethibitisha kupiga shoo katika tuzo hizo.

Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa Jumamosi ya Julai 18, 2015 huko KwaZulu-Natal, Afrika Kusini ambapo Tanzania inawakilishwa na wasanii wawili Vanessa Mdee na Diamond Platnumz.
Hawa ndiyo washiriki wetu katika tuzo hizo:

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA