Posts

CUF WATOA TAMKO ZANZIBAR

Image
Kaimu Mkurugenzi wa habari, uenezi na mawasiliano kwa umma Ismail Jussa. Kufuatia taarifa iliyotolewa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho iliyokutana Zanzibar juzi, tarehe 27 Desemba, 2015, waandishi wengi wa habari wametupigia simu wakitaka kujua Chama Cha Wananchi (CUF) kimepokea vipi taarifa ile. Vikao vya CCM ni vikao vya CCM. Si kawaida yetu kutolea taarifa maamuzi ya vikao vya vyama vyengine. Hata hivyo, tunaelewa ni kwa nini kumekuwepo na shauku ya kusikia CUF inasema nini kwa sababu yale yaliyokuwemo kwenye taarifa hiyo yaligusia pia mazungumzo yanayofanyika Ikulu Zanzibar yanayolenga kupata ufumbuzi wa mgogoro wa uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Oktoba, 2015. Baada ya kuipitia taarifa ya CCM na mengine yaliyoelezwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Zanzibar wakati akitoa ufafanuzi wa yale yaliyomo kwenye taarifa hiyo, CUF tunapenda kuwaeleza Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla haya yafuatayo: ...

NAPE KUZINDUA FILAMU YA ‘HOMECOMING’ UKUMBI WA CENTURY CINEMA

Image
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye leo anazindua filamu ya Homecoming katika Ukumbi wa Century Cinema uliopo Mlimani City. Mwongozaji wa filamu hiyo, Seko Shamte. Mwigizaji Mkuu wa Filamu hiyo Daniel Kijo. WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye jana amezindua filamu ya Homecoming katika Ukumbi wa Century Cinema uliopo Mlimani City. Uzinduzi huo pia ulioneshwa moja kwa moja na king’amuzi cha Azam kupitia Channel yake ya Sinema Zetu. Akizungumza kuhusiana na filamu hiyo mwongozaji wake Seko Shamte alisema kuwa filamu hiyo inahusiana na masuala ya rushwa na  imekuja wakati mwafaka ambapo jami imezinduka na kupambana na janga hilo. Alisema kuwa kwa sasa ni uzinduzi tu na kisha itaanza kuoneshwa kwa kulipia katika kumbi za Cinema kuanzia Januari 29 mwakani. Alisema kuwa wapenzi wa filamu wanaweza kufuatilia uzinduzi huo katika chanel ya Sinema Zetu ya King’amuzi cha Azam na kuongeza kuwa ni filamu ambayo inasisimua kuang...

TIGO YAFIKIA WAFUASI MILIONI MOJA KATIKA MTANDAO WA FACEBOOK

Image
Kampuni ya Tigo Tanzania hivi karibunii metangaza kufikisha wafuasi milioni moja katika mtandao wao wa Facebook. Katika ukarasa wake wa Facebook,  www.facebook.com/TigoTanzania    kampunii lifikisha mfuasi wa milioni moja Jumapili Desemba 27 mwaka huu hapa Tanzania. Kutokana na ongezeko la matumizi ya mtandao wa kijamii wa Facebook hapa nchini, Facebook imekuwa mstari wa mbele katika matumizi kutokana uzinduzi wa Facebook katika lugha ya Kiswahili uliofanyika mwaka wa 2014 kwa ushirikiano wa Tigo Tanzania na Facebook, ambapo wateja wanaweza  kutumia  Facebook kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza kupitia simu zao za mkononi bila malipo yoyote ya ziada. Ukurasa wa Facebook wa Tigo uliundwa Juni 2011 na umekuwa jukwaa madhubuti wa kurambaza na wateja wake wapendwa ambapo wanajifunza kuhusu huduma na bidhaa mpya za  kampuni. Hivi karibuni, Tigo Tanzania imejishindia   tuzo mbili katika Tuzo za Uongozi Bora (Tanzania Leadership Awards) ambay...

Taarifa ya Wizara kuhusu "mavazi na uvaaji usioruhusiwa"

Image
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo inapenda kuujulisha Umma kwamba kumekuwapo na upotoshwaji unaondelea katika mitandao ya kijamii hususan facebook, Instagram na WhatsApp ambapo sehemu ya upotoshaji huo imenukuliwa kama ifuatavyo “Wizara imetoa tamko kuwa kuanzia januari 2016 mavazi yote yasiyo stahiki ambayo hayaendani na mila na desturi zetu Wizara yangu na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haitafumbia macho mavazi hayo. HAYARUHUSIWI KUVALIWA SEHEMU ZIFUATAZO Kwenye masoko makubwa Hospitali kubwa(Private or Public) Maofisini na Vyuoni Mijini kwenye mikusanyiko ya watu wengi Hatua kali za kisheria zitachukuliwa endapo kwa wale ambao watavaa mavazi haya ikiambatana na faini ya sh. 100,000/=” mwisho wa kunukuu. Tunachukua fursa hii kukanusha vikali taarifa hizo kuwa siyo za kweli na kwamba mhusika amefanya uhalifu wa kimtandao kwa kuaanda taar...

BURUNDI: UFUNGUZI WA MAZUNGUMZO KATIKA HALI YA MVUTANO

Image
Na RFI Mkutano kati ya serikali ya Bujumbura, upinzani na vyama vya kiraia umeanza umechelewa, lakini mazungumzo hayo yamefunguliwa rasmi nchini Uganda, chini ya upatanishi wa rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni. Mazungumzo hayo yalikua yamesimama kwa muda wa miezi mitano. Mazungumzo ambayo ni moja ya njia ya kumaliza mgogoro unayoikumba Burundi tangu rais Pierre Nkurunziza kutangaza kuwania muhula wa tatu katika uchaguzi wa urais. Sherehe zimefanyika katika ukumbi wa Ikulu ya rais katika mji wa Entebbe, nchini Uganda, pamoja na wawakilishi wa serikali, upinzani na vyama vya kiraia. Pande zote zimeketi kwenye meza moja chini ya shinikizo la kimataifa. Watu zaidi ya mia moja, vyama kumi na tano, vimekuwepo Jumatatu hii asubuhi katika kikao cha ufunguzi wa mazungumzo hayo ili kila upande sauti yake isikike. Uwepo wao katika mji wa Entebbe umeonyesha matumaini, licha ya kutokea kwa mvutano na miguno kati ya wadau katika mgogoro huo. Rais wa Uganda ameanza kuwasilikiza was...

MAGAZETI YA LEO JUMANN, DECEMBER 29

Image

RAIS JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI AWAAPISHA MAWAZIRI ALIOWATEUA HIVI KARIBUNI

Image
Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni na Sanaa, Bi. Anastazia Wambura (kushoto) akisalimiana na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Mhe. Joyce Ndalichako (katikati) wakati wa sherehe ya kuapishwa kwa Mawziri wapya wanne ambao walikuwa bado hawajateuliwa na Rais, sherehe hizo zimefanyika leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Mawaziri wapya wakiwa tayari kuapishwa leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Mawaziri wapya wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya kuapishwa leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (kushoto) akimuapisha Mhe. Profesa Jumanne Maghembe (kulia) kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii,  leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. (P.T) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (kushoto) akimuapisha Mhe. Dkt. Joyce Ndalichako (kulia) kuwa  Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi. (Ni  baada ya kumteua kuwa Mbunge), leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. R...