UN: MAELFU YA RAIA WAMEUAWA IRAQ
Takriban watu milioni 3.2 wamelazimika kuhama makwao nchini Iraq Umoja wa Mataifa unasema kuwa ghasia zinazowakumba raia nchini Iraq ni nyingi huku takriban watu 18,800 wakiuawa kati ya tarehe mosi mwezi Januari mwaka 2014 na 31 mwezi Oktoba mwaka 2015. Takriban watu milioni 3.2 wamelazimika kuhama makwao ndani ya nchi katika kipindi hicho kulingana na ripoti mpya ya UN. Umoja wa mataifa unawalaumu wanamgambo wa Islamic State kwa kuendesha ghasia na kuwashikilia watumwa watu 3,500, wengi wakiwa ni wanawake na watoto. Islamic state wanawashikilia watumwa 3,500 wengi wakiwa ni wanawake na watoto Kamishna mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na haki za binadamu Zeid Raad Al Hussein anasema ripoti hiyo inaonyesha kile wakimbizi kutoka Iraq wanatoroka wakati wanakimbilia Ulaya na maeneo mengine. Ripoti hiyo inatokana na mahojiano na wale waliohama makwao na ushuhuda wa moja kwa moja kutoka kwa waathiriwa au wale walioshuhudia ukiukaji wa haki za binadamu Ripoti hiyo i...