BURKINA FASO: ZOEZI LA KUWATAMBUA WAHANGA LAENDELEA

Polisi wa Ufaransa wanachunguza gari lililochomwa moto mbele ya hoteli ya Splendid katika mji wa Ouagadougou, Burkina Faso, Januari 17, 2016.

Polisi wa Ufaransa wanachunguza gari lililochomwa moto mbele ya hoteli ya Splendid katika mji wa Ouagadougou, Burkina Faso, Januari 17, 2016.
Na RFI
Baada ya mashambulizi dhidi ya hotli ya Splendid na mgahawa wa Cappuccino katikati mwa mji mkuu wa Burkina faso, Ouagadougou siku ya Ijumaa usiku, wachunguzi wanaendelea na kazi ngumu ya kuwatambua watu 29 waliouawa katika shambulio hilo.
Mpaka sasa giza bado linatanda kuhusu namna operesheni ya vikosi vya usalama ilivyoendeshwa.
Mwendesha mashitaka wa Mahakama Kuu ya Ouagadougou, Maïza Sérémé, ametoa sehemu ya orodha ya watu waliopoteza maisha katika mashambulizi hayo ya kigaidi yaliyolenga hoteli ya Splendid na migahawa ya Cappuccino na Taxi Brousse.
Kati ya wahanga 29 waliohesabiwa, saba bado hawajatambuliwa, ikiwa ni pamoja na watu wanne weusi na wazungu watatu. Kati ya wahanga 22 waliotambuliwa, kuna wanne kutoka Canada, saba wa Burkina Faso, wawili kutoka Ukraine, Mfaransa mmoja mwenye asili ya Ukraine, Wafaransa wawili, wawili kutoka Uswisi, mmoja kutoka Libya, mmoja kutoka Marekani, mmoja kutoka Uholanzi na mmoja kutoka Ureno.
Mwendesha mashitaka, katika taarifa yake ya pili, amefahamisha raia na familia za wahanga kwamba uchunguzi wa kitabibu unaendelea na taarifa ijayo itawaitisha kuendelea na zoezi la kuwatambua wahanga na kuondolewa kwa miili yao.
Kukusanya ushahidi
Kuhusu uchunguzi, timu ya kiufundi bado ipo katika eneo la mashambulizi. Hairuhusiwi mtu yeyote kuingia katika sehemu kulikotokea mashambulizi. Maafisa wa polisi wanaendelea kukusanya vitu vyote ambavyo vinaweza kusaidia katika uchunguzi huu.(P.T)

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA