DC wa Kinondoni Salum Hapi akizungumza leo ofisni kwake NA BASHIR NKOROMO Mkuu wa Wilaya a Kinondoni, Dar es Salaam, Salum Hapi amesema, Serikali katika wilaya hiyo imebaini kuwa imepoteza zaidi ya sh. bilioni 1.331 kwa kuwalipa wafanyakazi hewa wapatao 89.hadi sasa. Amesema, baada ya kuapishwa kuwa mkuu wa wilaya hiyo siku saba zilizopita, amesimamia maofisa wake kufanya uchunguzi na kubaini kuwa pamoja na wafanyakazi hao hewa ambao wameisababishia serikali kupoteza sh. 1, 331, 734, 881 pia wapo watumishi vivuli wapatao 8823 ambao wanalipwa mishahara wakati hawafanyi kazi katika maeneo husika kutokana na sababu mbalimbali. Hapi amesema wafanyakazi hao vivuli ni pamoja na waliohamia idara nyingine lakini wakati wanalipwa huko walikokwenda bado wanalipwa katika idara walizokuwepo mwanzo na kwamba wengi wao wapo katika Idara ya Elimu. Akzungumza na waandshi wa habari Ofisini kwake, leo, Hapi amesema, amebaini hatua hiyo baada...