TIGO, MGAHAWA WA SAMAKI SAMAKI WAINGIA UBIA
Meneja wa Huduma za Masoko Tigo, Olivier Prentout (kushoto) akiongea na wanahabari wakati wa kusaini mkataba wa ushirikiano wa kibiashara kati ya kampuni ya simu za mkononi ya Tigo na Mgahawa wa Samaki samaki. Kulia ni Afisa Mkuu wa Maendeleo wa Mgahawa Samaki samaki, Saum Wengert.
Meneja wa Huduma za Masoko wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Olivier Prentout (kushoto) akiwa na Afisa Mkuu wa Maendeleo wa Mgahawa wa Samaki samaki, Saum Wengert wakionyesha mkataba wa ushirikiano wa kibiashara waliosaini kati ya kampuni ya Tigo na Mgahawa huo kwa waandishi wa habari jana jijini Dar Es salaam.
Kampuni ya simu inayoongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali ya Tigo Tanzania, leo imeingia ubia na mgahawa ya Samaki Samaki ambao ilianzishwa tangu mwaka 2007 ukiwa na matawi matatu yaliyopo Mlimani City, City Centre na Masaki Jijini Dar es salaam, ambapo pande hizo mbili zimekubaliana kufanya kazi pamoja kwa kuleta bidhaa/huduma zao kwa wateja wa kila mmoja.
Akitangaza ubia huyo jijini Dar es salaam leo, Meneja wa Huduma za Masoko wa Tigo Oliver Prentout aliviambia vyombo vya habari kuwa ushirikiano huo ni moja ya alama ambazo zinajenga imani kwamba wateja wa Tigo ambao sasa wanaweza kujitambulisha kupitia migahawa ya Samaki Samaki Tigo imeweka mtandao wa 4G LTE kwenye migahawa yote yaSamaki Samaki ili kuwawezesha wateja wake kufurahia intaneti ya kasi na ya haraka wakati wakila na kunywa kwenye migahawa hiyo inayouza vyakula vinavyotokana na mazao ya baharini hapa nchini.
“Tunaamini ushirikiano wetu utandelea kuonesha ni jinsi gani tumejikita kwenye kuboresha mabadiliko kwenye mtindo wa maisha ya kidijitali na kuongoza kwenye kutoa teknolojia ya kisasa na ubunifu kwa wateja wetu, alisema Meneja Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez.
Aidha Muasisi na Mkurugenzi wa migahawa ya Samaki Samaki, Bw. Carlos Bastos alisema Samaki Samaki wanawafanyia kazi Watanzania na wameungana na Tigo ambayo ni kampuni ya simu inayooongoza kwa ubunifu nchini kuwapatia wateja wake kile ambacho wamekisubiri kwa muda mrefu kwa jinsi huduma za Tigo zilivyo hususani uzoefu kwenye mtandao wa bure na wa kasi wa intaneti.
Kwa ushirikiano huu tutawapatia wateja wetu miradi mingi mipya, maboresho pamoja na ofa. Kufanya kazi na Tigo sio kwamba kunahusu sisi kupata fedha tu, bali inahusu ni nini cha ziada tunachoweza kuwapatia wateja wetu na hali kadhalika ni kwa kiasi gani tunaweza kujifunza kufanya kazi pamoja na kampuni iliyo na uzoefu mkubwa na ya kimataifa.
Tunaweza kuwa ni mgahawa unaoongoza kwa vyakula vinavyotokan na mzao ya baharini, lakini tunapenda kufanya jambo zaidi kwa ajili ya wateja wetu. Huduma za Tigo zinazotarajiwa kuwepo kwenye migahawa ya Samaki Samaki ni pamoja huduma ya bure ya intaneti bila nyaya (WiFi), Tigo Pesa na Tigo Music.
Comments
Post a Comment