Madaktari Bingwa waendelea kuwahudumia wananchi Singida
Baadhi ya wakazi wa Iramba waliojitokeza siku ya siku ya kwanza ya huduma tembezi za kibingwa. Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J. Mtigumwe akihutubiwa wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma tembezi za madaktari bingwa Mkoani Singida. Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida John Mwombeki akisoma taarifa ya hali ya afya Mkoa wa Singida wakati wa uzinduzi wa huduma tembezi za kibingwa Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Macho akimhudumia mteja siku ya kwanza ya huduma tembezi za kibingwa. Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Meno akimhudumia mteja siku ya kwanza ya huduma tembezi za kibingwa. Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J. Mtigumwe amezindua rasmi huduma tembezi za madaktari bingwa Mkoani Singida, na kuwasihi wananchi Mkoani Singida kujitokeza kwa wingi kupata huduma hizo za kibingwa. Huduma hizo za kibingwa zilizozinduliwa Wilayani Iramba katika hospitali ya Kiomboi zitahusisha huduma za kibingwa za upasuaji, meno, macho, upasuaji wa mif...