Muhimbili Yafanikisha Upasuaji Mfumo wa Njia ya Mkojo kwa Watoto Pacha
Daktari
bingwa wa upasuaji wa watoto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
(MNH, Dk Victor Ngotta (kushoto) akimfanyia upasuaji Eliudi jana kwa
kushirikiana na Profesa Saber Waheeb (katikati) na Dk Mohamed Malak
kutoka Misri (kulia).
Dk
Mohamed Malak, Profesa Saber Waheeb kutoka Misri na Dk Victor Ngotta
wakiendelea na upasuaji jana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
(MNH).
Daktari
Bingwa Watoto wa Upasuaji, Dk Zaituni Bokhary akizungumza jambo baada ya
kumfanyia upasuaji mtoto Elikana aliyekuwa na tatizo la mfumo wa njia
ya mkojo jana.
Dk Bingwa
wa Upasuaji, Dk Yona Ringo akiwa ofisini baada ya kumfanyia upasuaji
mtoto Elikana ambaye alikuwa na tatizo la mfumo wa njia ya mkojo jana.
Na John Stephen MNH
Hospitali
ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jana imefanikisha kuwafanyia upasuaji
watoto pacha ambao walikuwa wana tatizo katika njia mkojo.
Watoto
hao wametoka katika chumba cha upasuaji salama na sasa wanaendelea
vizuri baada ya kurejeshwa wodini. Watoto hao ni Eliudi Joel na Elikana
Joel ambao wana umri wa miaka mitatu kila mmoja.
Daktari
Bingwa Watoto wa Upasuaji, Dk Zaituni Bokhary na Dk Bingwa wa Upasuaji,
Dk Yona Ringo wamefanikisha upasuaji wa Elikana wakati Eliudi amefanyiwa
upasuaji na Profesa Saber Waheeb na Dk Mohamed Malak kutoka Misri kwa
kushirikiana na Dk Victor Ngotta na Dk Mwajabu Mbaga wa Muhimbili.
Dk
Bokhary amesema kuwa upasuaji wa watoto hao umechukua saa moja na nusu
na kwamba hivi sasa wanaendelea vizuri baada ya shughuli hiyo.
“Watoto hawa wataendelea kuwapo wodini hadi watakapopona vizuri ndio tutawaruhusu,” amesema Dk Bokhary.
Dk Bokhary amesema kuwa watoto wengine wawili jana wamefanyiwa upasuaji ambao walikuwa na tatizo kama hilo.
Juzi madaktari wa hospitali hiyo walianza upasuaji kwa watoto wenye matatizo ya njia ya mkojo na mfumo wa hewa na chakula
Comments
Post a Comment