Posts

Uingereza kuwabana wanafunzi wa kigeni

Sheria kali zilizoanzishwa nchini Uingereza kuhusu wanafunzi kutoka nje ya ulaya wanaokuja nchini humo kwa masomo zitawafanya wanafunzi wengi kutoka barani Afrika kutoweza kusomea Uingereza. Idara ya uhamiaji Uingereza - UK Border Agency, imesema watu wengi wametumia vibaya na kukiuka sheria za uombaji wa viza hasa za wanafunzi. Serikali ya Uingereza imeongezea vikwazo kupiga vita ukiukaji wa sheria hizi. Ukiukaji wa sheria umekuwa ukifanyika kufuatia kukomeshwa kwa uchunguzi uliokuwa ukifanywa kuhakikisha kwamba wanafunzi wanarudi nchini mwao baada ya kumaliza masomo yao na mda waliopewa na idara ya uhamiaji Uingereza kumalizika. Ingawaje wanafunzi wanachunguzwa kabla ya kupewa viza, hawajakuwa wakichunguza hivi karibuni kuhakikisha kwamba wamerudi nchini mwao.Imekuwa vigumu kujua idadi ya wale wanaorudi na wale wanaoishi Uingerza kinyume cha sheria. Idara ya uhamiaji inasema kwamba itakuwa vigumu sana kuvunja sheria za uhamiaji siku zijazo. Mnamo mwaka 2011, Idara hio itakuwa na tech

Harusi ya wanaume yavunjwa Mombasa

Polisi katika mtaa wa Mtwapa ulioko kaskazini mwa mji wa Mombasa nchini Kenya wamewakamata wanaume wawili waliokuwa wanajiandaa kuoana. Afisa wa utawala katika eneo hilo George Matundura amesema wanaume hao walikuwa na pete tayari kufunga ndoa katika hoteli moja iliyoko Kikambala katika wilaya jirani ya Kilifi. Raia pia wameripotiwa kuwakamata wanaume wengine kadha wanaodaiwa kushiriki mapenzi ya jinsia moja na kuwakabidhi kwa Polisi. Ndoa za watu wa jinsia bora ni marufuku nchini Kenya, lakini sio jambo la kawaida wale wanaofanya hivyo kukamatwa. Makundi ya Waislamu na Wakristo katika eneo hilo walifanya maandamano wakilaani kile walichokielezea kuwa tabia ya baadhi ya watu isiyokubalika katika eneo hilo la Mtwapa.

MIRIAM APANDISHWA KIZIMBANI LEO

Image
Miss Tanzania 2009 Miriam Gerald na Boyfriend wake Kenedy amepandishwa kizimbani leo kwenye mahakama ya Wilaya Kinondoni akishitakiwa kwa kosa la kufanya vurugu na kuharibu mali za bendi ya Volcano Sound inayomilikiwa na mwanamuziki Taji Mbaraka mtoto wa Marehem Mraka Mwishehe kwenye ukumbi wa TPDC Mikocheni. Kesi hiyo iliyofunguliwa Oysterbay na ilikuwa na jalada na OB /RB/2267/010 KUHARIBU MALI NA SHAMBULIO imesomwa leo katika mahakama hiyo na mshitakiwa Miriam amewekwa mahabusu ya mahakama hiyo baada ya kukosa dhamana, kesi imaeahirishwa, hata hivyo ndugu na jamaa wanahangaika ili kuhakikisha anapata dhamana kabla muda wa kuwachukua mahabusu kutimia ili kuweza kumnasua na kupata dhamana, bado haijafahamika kama ataweza kutimiza masharti ya dhamana na kufanikiwa kupata kwa leo au la. Kimsingi kama Miriam atapatikana na hatia hii itakuwa ni jambo baya kwa mrembo huyo anayeshilikila taji la Miss Tanzania 2009/2010 kwakuwa mrembo huyo aliaswa na wadau mbalimbali wa urembo kuwa balozi mw

MPANGO MZIMA WA MAANDALIZI YA "ZINDUKA"LEADERS CLUB"

Image
MAANDALIZI YAKIENDELEA KATIKA VIWANJA VYA LEADERS JIJINI DAR ES SALAAM AMBAPO TAMASHA KUBWA KABISA LA "ZINDUKA" LITAZINDULIWA HAPA KWA NIA MOJA TU YA KUTOKOMEZA UGONJWA WA MALARIA,MHESHIMA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DR.JAKAYA MRISHO KIKWETE NDIO ATAZINDUA RASMI.KUTAKUWA NA BURUDANI PIA KUTOKA KWA WASANII MBALIMBALI WA BONGO FLAVOUR KAMA VILE LADY JAY DEE,MATALUMA,PROFESA JAY,BANANA ZORO,MWASITI,BI KIDUDE,RAY C,KIINGILIO NI ELFU 3000 TU."the source of pictures are from www.michuzijr.blogspot"

HII MIKAO MINGINE INA MAANA HAWAWEZI KUKAA CHINI?

Image
Hawa askari wa jiji wana hatari unacheki walivyokalia virungu vyao!iga uone

LIL WAYNE ACHUNGULIA JERA:

Image
Haya ni maneno aliyoyasema lil wayne jana baada ya hukumu yake kuhairisha kutokana na kesi inayomkabili ya kukutwa na bunduki kinyume cha sheria I'm out this b----. To all my fans, my real fans I really, really truly love you. I love you with all of me for real. Tonight's my last night. ... I came to the studio to get some work done. To all you artists out there, that should be a message or example. I came to work. For all the people that didn't know, this is the last time you gonna be seeing me live for a long muthaf---in' time. So watch: This is history."

UMEKIONA KITU CHA KICHINA?

Image
Dah hips za k........ tutasalimika kweli? ukimwi utatumaliza chukua hatua tulia na wako.BROTHERS AND SISTERS

SASA WE DOGO NDO...............

Image
SI watoto wa kibongo tu wanavisa cheki huyu dogo wa majuu ina maana hana njaa ya siku mbili?
Image
wakazi wa zenj mkae tayari kwa kumpokea kijana anayetisha kwenye game la bongo flavour kwa zile nyimbo za malavi davi

HOTEL MALTIVILA

Image
Unapokuwa mji wa musoma(MSM TOWN)Basi hapa ndo mahali pa kupata mlo wako,wanapatikana mtaa wa mukendo kubwa ilipokuwa RTC zamani

ZINDUKA KUFANYIKA TAREHE 13/02/2010

Image
(ZINDIUKA) kampeni ya kutokomeza malaria ambayo itazinduliwa februari 13 kwa onyesho kubwa litakalofanyika kwenye viwanja vya Leaders Kionondoni jijini Darisalaam. Mgeni wa heshima akiwa Rais Jakaya Kikwete, kampeni hiyo itaendeshwa karibu nchi nzima, pia kampeni hii ni kuhamasisha kizazi kipya cha vijana kupambana na ugonjwa wa malaria ili kuifanya jamii iliyo salama dhidi ya ugonjwa huo hapa nchini na inaratibiwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii pamoja na mradi wa kutokomeza maralia.b wasanii kibao atakuwepo ikiwa ni pamoja na kidumu kutoka burundi,lady jay dee, pro jay, diamond, dully,marlow,madee,jeska, bi kidude, mwasitimataluma, triple x, banana, ngwea na wengine kibao..

ONA VITU OBAMA ALIVYOTUPIA

Image
Obama ni soo kwa bling bling katupia vitu vya ukweli si unaona we mwenyewe.