MIRIAM APANDISHWA KIZIMBANI LEO


Miss Tanzania 2009 Miriam Gerald na Boyfriend wake Kenedy amepandishwa kizimbani leo kwenye mahakama ya Wilaya Kinondoni akishitakiwa kwa kosa la kufanya vurugu na kuharibu mali za bendi ya Volcano Sound inayomilikiwa na mwanamuziki Taji Mbaraka mtoto wa Marehem Mraka Mwishehe kwenye ukumbi wa TPDC Mikocheni.
Kesi hiyo iliyofunguliwa Oysterbay na ilikuwa na jalada na OB /RB/2267/010 KUHARIBU MALI NA SHAMBULIO imesomwa leo katika mahakama hiyo na mshitakiwa Miriam amewekwa mahabusu ya mahakama hiyo baada ya kukosa dhamana, kesi imaeahirishwa, hata hivyo ndugu na jamaa wanahangaika ili kuhakikisha anapata dhamana kabla muda wa kuwachukua mahabusu kutimia ili kuweza kumnasua na kupata dhamana, bado haijafahamika kama ataweza kutimiza masharti ya dhamana na kufanikiwa kupata kwa leo au la.
Kimsingi kama Miriam atapatikana na hatia hii itakuwa ni jambo baya kwa mrembo huyo anayeshilikila taji la Miss Tanzania 2009/2010 kwakuwa mrembo huyo aliaswa na wadau mbalimbali wa urembo kuwa balozi mwema kwa Nchi, jamii na kwa kamati ya Miss Tanzania .
habari zaidi tutawaletea baadae

taarifa hii ni kwa hisani ya "JOHN BUKUKU" kutoka blog ya www.fullshangwe.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA