HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA USIKU WA SERENGETI FIESTA NDANI YA MUSOMA
Msanii mwingine anaefanya vyema hivi sasa katika anga ya muziki wa Bongofleva,Rich Mavoko akiwaimbisha mashabiki wake usiku huu,mbele ya wakazi wa mji wa musoma waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013,ndani ya uwanja wa Karume mkoani Mara. Madansa wa msanii wa muziki wa kizazi kipya,Shilole wakitumbuiza jukwaani usiku huu ndani ya Uwanja wa Karume,ndani ya mji wa Musoma mkoani Mara,ambapo tamasha la serengeti fiesta 2013 likiendelea hivi sasa. Anajiita tajiri wa Mahaba Cassim Mganga kutoka Manzabay akiwaimbisha jukwaani wakazi wa mji wa Musoma,wakati tamasha la serengeti fiesta 2013 likiendelea hivi sasa ndani ya uwanja wa Karume. Mashabiki wakijinafasi kwa raha zao. Kundi la Wanaume TMK likiongozwa na Chege na Temba wakilishambulia jukwaa la serengeti fiesta usiku huu ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani Mara. Mkali mwingine wa muziki wa Reggae kutoka kanda ya Ziwa,Jita Man akiwakumusha mash