SUMATRA YASITISHA SAFARI ZIWA VICTORIA KWA ABIRIA WASIO NA VITAMBULISHO.

SUMATRA YASITISHA SAFARI ZIWA VICTORIA KWA ABIRIA WASIO NA VITAMBULISHO.

Mamlaka ya Uthibiti Usafiri wa nchi kavu na Majini SUMATRA, imewataka abiria na wananchi wote wanaotumia vyombo vya usafiri wa majini kupitia Bandari zote za Ziwa Victoria , kuwa na kitambulisho kinachoonyesha taarifa zao mhimu wakati wa kukata tiketi.
Akitoa taarifa hiyo hiyo hii leo Mkoani Mwanza, Mhandisi Japhet Loisimaye Ole ambae ni Afisa Mfawidhi wa SUMATRA Kanda ya Ziwa kwa niaba ya Msajili wa Meli SUMATRA, Amesema kwamba utaratibu huu unalenga kuwa na taarifa sahihi kwa kila abiria katika meli ama boti, sambamba na kuzuia abiria kusafiri kwa kutumia tiketi yenye jina la mtu mwingine.
Amesema kwamba utaratibu huo kwa kanda ya ziwa utaanza kutumika rasmi kuanzia leo septemba 9, ambapo wamiliki wa Meli ama Boti watalazimika kujaza taarifa sahihi katika orodha ya wasafiri kwa mujibu wa vitambulisho vyao.
 Mhandisi Ole amebainisha kwamba kupitia utaratibu huo, Maafisa wa Bandari na Mialo yote iliyoko ndani ya Ziwa Victoria watawaruhusu abiria wenye tiketi halali na vitambulisho husika pekee kuingia bandarini ama melini.
Ameainisha vitambulisho vinavyoweza kuwasilishwa ni pamoja na Kitambulisho cha uraia, Kitambulisho ukaazi,Hati ya kusafiria (Passport), Kitambulisho kupigia kura,kitambulisho cha kazi, leseni ya udereva pamoja na barua ya utambulisho inayotolewa na serikali za mitaa yenye picha.
 Amefafanua kwamba kwa upande wa watoto wadogo ambao wengi wao hawana vitambulisho vya aina yoyote, watatumia barua za utambulisho zinazotolewa na serikali za mitaa, barua ambazo sharti ziwe na picha ya mhusika.
Aidha amebainisha kwamba agizo hilo halitawahusu abiria wanaotumia usafiri wa meli ama boti zinazosafiri umbali usiozidi maili za majini 20 kati ya bandari moja na nyingine sambamba na vivuko kwa maana ya Ferry.
Katika hatua nyingine Mhandisi Ole amesema kwamba suala la kuonyesha vitambulisho halina gharama yoyote na hivyo kuwataka kuonyesha ushirikiano wao, huku akitoa onyo la kuwachukulia hatua kali wamiliki wa vyombo vya usafiri wa majini watakaokuwa wanasafirisha abiria kinyemera bila kufuata utaratibu huo.
Agizo hili limekuja ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Kanuni za Kuhakiki na Kusajiri Abiria (Mechant Shipping Counting and Regstration of Person on Board Passenger Ships) kama zilivyoainishwa na tangazo la serikali Na: 142/2011, likiwa na lengo la kupata idadi na taarifa kamili za abiria, taarifa ambazo husaidia katika wokozi pindi chombo cha usafiri kinapopata dharura majini.
source gsengoblog

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA