Posts

VICHWA VYA MAGAZETI LEO JUMANNE HIVI HAPA

Image

AUDIO: Sikiliza na kudownload brand new single kutoka kwa Gosby Feat. Ommy Dimpoz-" Naogopa"

Image

CHRIS BROWN KUENDELEA KUSOTA JELA ZAIDI BAADA YA KUKIUKA MASHARTI

Image
Brown alifungwa jela baada ya kumchapa aliyekuwa mpenzi wake Rihana Mwanamuziki wa Marekani Chris Brown atasalia jela kwa siku nyingine 131 baada ya kukiri kukiuka amri ya mahakama kuhusu kifungo cha nje alichokuwa amepewa na mahakama. Muimbaji huyo wa muziki wa mtindo wa R&B alikiri mahakamani mjini Los Angeles mnamo siku ya Ijumaa kuwa alitenda uhalifu mjini Washington Oktoba mwaka jana. Jaji alimuhukumu kifungo cha siku 365 jela ingawa alimpongeza kwa kuhudumia siku 234 katika kituo cha kupata ushauri nasaha. Brown amekuwa chini ya aungalizi wa mahakama tangu mwaka 2009 alipokiri kumpiga mwanamuziki mwenza na ambaye alikuwa mpenzi wake wakati huo,Rihanna. Mshindi huyo wa tuzo la Grammy amekuwa kizuizini tangu mwezi Machi alipokamatwa kwa kukiuka amri ya mahakama iliyomweka ndani ya kituo cha ushauri nasaha pamoja na jela.

VIDEO:HII NDO VIDEO ALIYOITOA EMINEM SIKU YA MAMA DUNIANI AKIMWOMBA MSAMAHA MAMA YAKE

DAKTARI BIGWA WA MAGONJWA YA AKILI AFARIKI KWA DENGUE

Image
Waombolezaji wakimfariji Leticia Filbert, mke wa daktari bingwa wa Hospitali ya Temeke, marehemu Dk Gilbert Buberwa nyumbani kwake Kinyerezi, Dar es Salam jana. Picha na Salim Shao   chanzo cha habari mwananchi. Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Akili nchini, Gilbert Buberwa amefariki dunia kutokana na ugonjwa wa dengue. Kifo cha Dk Buberwa kinafanya idadi ya watumishi wa afya waliofariki dunia kutokana na ugonjwa huo kufikia wawili baada ya muuguzi Hamida Likoti kufariki dunia wiki iliyopita. Ugonjwa huo uliolipuka mkoani Dar es Salaam, umezua taharuki kwa wakazi wake kwa sababu hauna tiba na unasababishwa na mbu, Aedes Egyptae, anayeuma mchana na anayeweza kuzaliana katika majisafi yaliyotuama. Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk Primus Saidia alisema jana kuwa Dk Buberwa alifariki dunia saa saba usiku wa kuamkia jana akiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH). Dk Buberwa alianza kuumwa ugonjwa huo a

VICHWA VYA MAGAZETI LEO JUMATATU

Image