CHRIS BROWN KUENDELEA KUSOTA JELA ZAIDI BAADA YA KUKIUKA MASHARTI
Mwanamuziki wa Marekani Chris
Brown atasalia jela kwa siku nyingine 131 baada ya kukiri kukiuka amri
ya mahakama kuhusu kifungo cha nje alichokuwa amepewa na mahakama.
Muimbaji huyo wa muziki wa mtindo wa R&B
alikiri mahakamani mjini Los Angeles mnamo siku ya Ijumaa kuwa alitenda
uhalifu mjini Washington Oktoba mwaka jana.
Jaji alimuhukumu kifungo cha siku 365 jela ingawa alimpongeza kwa kuhudumia siku 234 katika kituo cha kupata ushauri nasaha.
Brown amekuwa chini ya aungalizi wa mahakama
tangu mwaka 2009 alipokiri kumpiga mwanamuziki mwenza na ambaye alikuwa
mpenzi wake wakati huo,Rihanna.
Mshindi huyo wa tuzo la Grammy amekuwa kizuizini
tangu mwezi Machi alipokamatwa kwa kukiuka amri ya mahakama iliyomweka
ndani ya kituo cha ushauri nasaha pamoja na jela.
Kifungo alichopata kuongezewa siku kinahusiana na kisa cha ugomvi kilichotokea mjini DC mwaka jana.
Brown anakabiliwa na mashitaka ya kumchapa mwanamume mmoja nje ya hoteli moja mjini Washington
Comments
Post a Comment