MREMBO AMCHOMA VISU MBONGO SAUZI
Stori: Mayasa Mariwata na Shani ramadhani WIVU wa mapenzi bwana! Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la David Patrick Chagu (pichani) aliyekuwa akiishi Jimbo la George nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’ amekumbwa na mauti kwa kuchomwa visu na mpenziwe aliyefahamika kwa jina moja la Monica. Waombolezaji na mama wa marehemu, Rose Ndunguru (wa pili kulia) wakiwa katika hali ya simanzi. Tukio hilo lilitokea Oktoba 2, mwaka huu na marehemu alizikwa Oktoba 14, mwaka huu katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar huku akiwa ameacha mtoto wa miezi nane. Marafiki wa karibu wakimuaga mpendwa wao marehemu David Patrick Chagu. Kwa mujibu wa chanzo, marehemu alichomwa visu na mpenzi wake huyo ambaye ni Mzungu kwa madai ya wivu kufuatia kutomwona kwa siku tatu na kumhisi ana mpenzi mwingine. Waombolezaji wengine wakiomboleza katika msiba huo wakati wa mazishi. Akizungumza na Uwazi kwa majonzi makubwa, mama mzazi wa marehemu, Rose Ndunguru ambaye ni Katibu wa Umoja wa Wanawake wa