Team Diamond vs Team Alikiba: Kinachoendelea Instagram Kinatutia Aibu Watanzania!
Upinzani kati ya Diamond Platnumz na Alikiba sasa unaelekea kubaya. Kiukweli nimesikitishwa sana na kile ambacho ninakiona kikiendelea kwenye Instagram kati ya kambi hizi mbili. Infact nahisi ushabiki huu una hasara nyingi kuliko faida kwenye industry yetu. Kwa leo sitaongelea jinsi ushabiki wa wasanii hawa wawili wenye nguvu unavyofanya wasanii wengine wanaofanya vizuri nchini kutoangaliwa, bali nitazungumzia kusikitishwa na kile kinachofanyika Instagram ambapo mashabiki wa Alikiba wameanzisha kampeni ya kuhakikisha kuwa Diamond anakosa tuzo kwenye MTV MAMA pamoja na mashabiki wa Diamond kumtukana Davido bila hatia! Kwanini lakini tunafanya hivi? Hivi kweli tunaamua kujidhalilisha kiasi hiki? Majirani zetu wanatucheka, wanatubeza, wanatushangaa kweli kweli! Ushindani huu wa ndani kati ya wasanii hawa wawili kwanini uondoe utaifa wetu? Ushabiki gani huu? Diamond Platnumz amechaguliwa kuwania vipengele vitatu kwenye tuzo za mwaka huu za MTV MAMA, iwapo akishinda, ushindi wake