MKURUGENZI MKUU WA TWITTER KUJIUZULU

Mkurugenzi Mkuu wa Twitter, Dick Costolo anayetarajia kujiuzulu.
Mkurugenzi Mkuu wa Twitter, Dick Costolo, ana nia ya kujiuzulu ifikapo Julai mosi, kufuatia shinikizo kutoka kwa wawekezaji, ambao wanalalamikia kukua polepole wa mtandao huo wa kijamii.
Baada ya kujiuzulu nafasi hiyo ya Mkurugenzi Mkuu, Costolo atabaki kuwa Mjumbe wa bodi ya Wakurugenzi wa kampuni hiyo.
Twitter imeshindwa kupata faida katika kipindi cha miaka tisa tangu ilipoanzishwa.
Mwanzilishi mwenza wa mtandao huo Jack Dorsey anatarjiwa kuchukua nafasi hiyo kama kaimu Ofisa Mkuu kuanzia Julai mosi na kukalia wadhifa huo hadi pale mrithi wake atakapochaguliwa.
Katika taarifa yake, Costolo amesema kuwa anafurahishwa na wafanyikazi wa kampuni hiyo.
Mnamo mwezi Aprili kampuni hiyo ilipata hasara ya dola milioni 162 hivyo kufanya ukuaji wa kampuni kushuka kwa kiwango kikubwa na kuathiri uwekezaji.
Bei ya hisa zake ilishuka kwa asilimia 30 na sasa zinaendelea kuuzwa kwa bei ya uanzilishi wake ya mwaka 2013.BBC

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA