MKWASA ATANGAZA KIKOSI CHA TAIFA STARS...KIPO HAPA
Kocha mpya wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa aliyechukua nafasi ya Mart Nooij ametangaza kikosi chake kipya kwa ajili ya kuivaa Uganda huku akimtema kipa Deogratius Munish ‘Dida’ na nafasi yake amemchagua Ally Mustapha ‘Barthez’. Wengine ambao Mkwasa amewatema ni Erasto Nyoni, Amri Kiemba na Kelvin Friday kutoka Azam FC pia Oscar Joshua kutoka Yanga, Pia Ibrahim Ajibu kutoka Simba. Waliorejea ni Kelvin Yondani pia Deus Kaseke huku akimchukua Michael Idan wa Ruvu Shooting. Pia Samuel Kamuntu wa JKT, Juma Abdul wa Yanga na Mudathir Yahya kutoka Azam wamejumuishwa kwamba wanaweza kuitwa wakati wowote. KIKOSI KAMILI: Mwadini Ally-Azam Ally Mustapha-Yanga Mudathir Khamis-KMKM Shomari Kapombe-Azam Michael Haidan-Ruvu Shooting Mohammed Hussein-Simba Mwinyi Hajj-KMKM Nadir Haroub-Yanga Kelvin Yondani-Yanga Aggrey Morris-Azam Hassan Isihaka-Simba Jonas Mkude-Simba Abdi Banda-Simba Simon Msuva-Yanga Said Ndemla-Simba Ramadhan Singano-