Posts

Breaking News: Bobbi Kristina mwanawe Whitney afariki

Image
Bobbi Kristina Brown ,mtoto wa marehemu Whitney Houston ambaye alikuwa gwiji wa muziki wa R&B ,amefariki dunia baada ya kupoteza fahamu kwa muda wa miezi sita tangu alipokutwa taabani kwenye bafu lake na pindi alipofikishwa hospitalini na kukutwa na matatizo kwenye ubongo. Bobbi amekufa akiwa na umri wa miaka 22,huku akivutiwa kuwa muigizaji na muimbaji mahiri na mwenye ubora wa aina yake. Msemaji wa familia Kristen Foster amesema Bobbi amefariki akiwa amezungukwa na familia yake ,''hatimaye yuko salama sasa kwenye mikono ya Mwenyezi Mungu,tunawashukuru wote walioungana nasi katika maombi na kuonesha upendo kwa miezi michache iliyopita''. Bobbi ambaye alikuwa amepoteza fahamu tangu akutwe ameanguka kwenye bafu lake panapo tarehe 31 januari mwaka huu na kuwekwa kwenye matibabu huku akiwa amekosa ufahamu na mpaka kifo chake kumkuta alikuwa hajapata fahamu bado. Inakumbukwa kuwa miaka mitatu iliyopita mama yake Bobbi,alikutwa pia kwenye bafu lake amepoteza fah

PICHA ZA ZARI AKIWA NA DIAMOND PLATINUMZ MPYA ZAWA GUMZO KWENYE MITANDAO YA KIJAMII

Image
Kwa raha zetu...... vaeni madera, fungeni mikanda mpite kimya kimya Keeping it sexy and classy. #BabyBumpPhotoShoot  CREDIT GOES TO @iviewstudios  and  @raqey_allaraqya

TUJIKUMBUSHE: BOMU LINALOMWANDAMA SAMIA SULUHU HASSAN

Image
Samia Suluhu Hassan Kisiwa cha utalii cha Changuu, kilikodishwa kwa ‘ bei chee’ na kampuni ya Leizure Hotel Limited, ripoti ya Kamati ya Baraza la Wawakilishi (BLW) imebaini. Ripoti ya Kamati ya BLW iliyoundwa kuchunguza ubadhirifu wa mali za serikali , imebaini kuwa kilikodishwa kwa kodi ya Dola 1,000 kwa mwezi na kumtaja aliyehusika na ukodishwaji huo kuwa ni aliyekuwa Waziri wa Utalii Biashara na Uwekezaji Zanzibar, Samia Suluhu Hassan. Waziri huyo wa zamani anatajwa kuwa alishirikiana na Kitengo cha Uwekezaji Zanzibar, (ZIPA) kufanikisha suala hilo Desemba 2002. Katika Baraza la Mawaziri la sasa Samia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano). Kwa mujibu wa ripoti hiyo kisiwa hicho chenye ukubwa wa hekta 11.27 kimekodishwa mwaka 2002 kwa malipo ya Dola za Marekani 1,000 kwa mwezi katika kipindi cha miaka 30. (Dola moja ni karibu sawa na Sh. 1,580) Hata hivyo kodi hiyo imerekebishwa na kufikia Dola 3,500 licha ya kwamba kabla ya kuwamilikisha wageni kisiwa hicho k

SOMA HABARI ZA MAGAZETI YA LEO JUMATATU, JULY 27

Image

HABARI ZA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI, JULY 25

Image
. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

Kajala afungukia kuingia kwenye siasa

Image
CHANZO:GPL Staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ‘Kay’ amefungukia kuingia kwenye siasa kuwa ni bora abaki kwenye upenzi na chama fulani kwani hawezi kugombea.   Akizungumza juzikati, Kajala alisema kuwa, japokuwa wasanii wengi wakiwemo wa tasnia ya filamu Bongo, wamekuwa wakichukua fomu za kutaka kugombea nafasi mbalimbali za udiwani na ubunge lakini kwake hafikirii kitu kama hicho. “Mimi siasa siiwezi kabisa, kifupi haipo kwenye damu ndiyo maana unaona wenzangu wote wamechukua fomu za kugombea mimi wala sijajitokeza kuchukua,” alisema Kajala.

Mwigizaji mwenye jina kubwa Riyama Ally Alilia Ndoa!

Image
chanzo: GL Mwigizaji mwenye jina kubwa ndani ya sanaa ya maigizo Bongo, Riyama Ally amekiri kutamani maisha ya ndoa huku akishikilia alichokisema ‘nasubiri wakati wa Mungu’.     Akizungumza na  Gazeti la  Amani  kwa njia ya simu hivi karibuni, msanii huyo mwenye sifa za kuvaa uhusika wa huzuni na kulia katika filamu nyingi, alisema akiwa mwanamke aliyekamilika, anahitaji kuwa na mume wake katika ndoa takatifu lakini akaweka wazi kuwa kwa sasa ana mchumba ambaye anamuomba Mungu usiku na mchana ili awe mumewe.   “Kila mtu aliyekamilika anahitaji maisha ya ndoa, hakuna kitu chenye heshima katika maisha ya binadamu kama kuwa na ndoa na kuishi kwa amani, lakini kila kitu hupangwa na Mungu. Kiukweli kabisa natamani sana ndoa, nina mchumba ambaye namuomba Mungu amfanye kuwa mume wangu,” alisema Riyama.