SELCOM YALETA MFUMO MPYA NA WA KISASA WA MALIPO YA TIKETI
Kwa mara ya kwanza nchini Tanzania wahudhuriaji wa tamasha la ‘KiliFest’ wataweza kutumia Selcom Card kupata tiketi za tamasha hilo lililoandaliwa na kampuni ya Bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambalo litafanyika siku ya Jumamosi September 26, 2015 katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es salaam. Kati ya mawakala wa Selcom zaidi ya 15,000 wanaopatikana nchi nzima ni mawakala 40 tu wameochaguliwa kuuza tiketi za KiliFest kwenye vituo vyao na wote hao wanapatikana Dar es salaam. Baada ya kulipia Tsh 10,000/- tiketi itawekwa moja kwa moja kwenye Selcom Card kwa njia ya kielektroniki ambapo mteja atakuwa amepata Selcom Card bure na atatakiwa kufika na kadi hiyo Leaders Club siku ya tamasha na kugonga (tap) kwenye mashine za POS za Selcom zitakazokuwa zinapatikana kwenye milango ya kuingilia ya Leaders Club ili kuhakikisha manunuzi ya tiketi. Selcom Card itamuwezesha mteja kupata tiketi za tamasha la KiliFest kwa sasa na kuitumia