SELCOM YALETA MFUMO MPYA NA WA KISASA WA MALIPO YA TIKETI

unnamed
Kwa mara ya kwanza nchini Tanzania wahudhuriaji wa tamasha la ‘KiliFest’ wataweza kutumia Selcom Card kupata tiketi za tamasha hilo lililoandaliwa na kampuni ya Bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambalo litafanyika siku ya Jumamosi September 26, 2015 katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es salaam.
Kati ya mawakala wa Selcom zaidi ya 15,000 wanaopatikana nchi nzima ni mawakala 40 tu wameochaguliwa kuuza tiketi za KiliFest kwenye vituo vyao na wote hao wanapatikana Dar es salaam. Baada ya kulipia Tsh 10,000/- tiketi itawekwa moja kwa moja kwenye Selcom Card kwa njia ya kielektroniki ambapo mteja atakuwa amepata Selcom Card bure na atatakiwa kufika na kadi hiyo Leaders Club siku ya tamasha na kugonga (tap) kwenye mashine za POS za Selcom zitakazokuwa zinapatikana kwenye milango ya kuingilia ya Leaders Club ili kuhakikisha manunuzi ya tiketi.

Selcom Card itamuwezesha mteja kupata tiketi za tamasha la KiliFest kwa sasa na kuitumia kadi hiyo hapo baadae kufanya malipo na manunuzi mbalimbali baada ya tamasha hilo.

Malipo na manunuzi yatakayoweza kufanyika kwa kutumia Selcom Card ni pamoja na malipo ya manunuzi ya bidhaa kwenye supermarkets, kulipia mafuta ya gari kwenye vituo vya mafuta, kulipia tiketi za matamsha yajayo, kulipia bili za chakula kwenye migahawa/bar, kupokea na kutuma pesa kwenda mitandao yote na kwenye akaunti za benki, kutoa pesa kwa wakala wa Selcom, kulipia tiketi za usafiri, bili za LUKU, DAWASCO, NHC, AzamTV, ZUKU, Startimes, DSTV, nk, kununua vifurushi vya internet pamoja na muda wa maongezi wa mitandao yote.

Hapo awali kumekuwa na changamoto kubwa wakati wa uuzaji wa tiketi za matamasha mbalimbali ambapo imekuwa ni vigumu kudhibiti wizi na tiketi feki, kwa kupitia mfumo huu mpya wa Selcom Card sasa waandaji wa matamasha wataweza kuzuia wizi wa tiketi na kuwa na uwezo wa kuuza tiketi mapema kabla ya tamasha na pia kuweza kujua nani ameingia kwenye tamasha hilo.

Lengo kuu la Selcom Card ni kuwarahisishia wananchi na kuwajengea utamaduni wa kufanya malipo mbalimbali kwa kutumia mfumo wa kadi ambao ni wa haraka, salama na uhakika bila kubeba fedha mkononi kila wanapohitaji kufanya malipo au mununuzi. Watumiaji wataweza kuongeza fedha kwenye kadi zao za Selcom (Salio) kwa mawakala wote wa Selcom nchini au kwa njia ya simu banking.

Selcom ni kampuni inayoongoza katika utoaji wa huduma mbalimbali za kifedha kwa njia ya simu za mkononi na yenye uzoefu mkubwa kwenye nyanja ya Teknolojia nchini Tanzania na ndio msingi wa uendeshaji wa huduma ya kifedha kwa njia ya simu ikishirikiana na mitandao yote minne ya simu hapa nchini, benki zaidi ya 30 na vituo vya mauzo vya Selcom vinavyotumia mashine za POS vilivyopo zaidi ya 15,000 nchi nzima. Pia Selcom ni wawezeshaji wa malipo na manunuzi ya huduma mbalimbali kwa washirika zaidi ya 50 kupitia simu za mkononi, simu banking na mawakala wake. Selcom ni kampuni inayoongoza Tanzania kwa kuanzisha huduma za malipo ya kielektroniki katika miji mbalimbali ya Afrika Mashariki na ni kampuni ya kwanza kuzindua malipo na manunuzi kwa njia ya kadi nchini Tanzania.

Selcom, Tunakuwezesha Kwa Njia Ya Teknolojia
+255 787 523152
www.selcom.net

SEHEMU ZINAPOPATIKANA TIKETI ZA KILIFEST
NO. SHOP NAME LOCATION DECRIPTION
1 Village Super Market Masaki Sea Cliff House Branch
2 Village Super Market Masaki Chole Road Branch
3 Village Super Market Mbezi Beach Tank Bovu Branch
4 Shrijee Supermarket Osterbay – Morogoro Store near Mohans Osterbay Branch
5 Shrijee Supermarket Masaki Masaki Branch

6 Shrijee Supermarket Kisutu – Mtendeni Street Kisutu Branch
8 Shoppers Supermarket Mikocheni – Shoppers Plaza Mikocheni Branch
9 Shoppers Supermarket Mbezi Beach – Kwa Street Mbezi Beach Branch
10 A to Z Supermarket Upanga – Ocean Road – Near Ocean Road Hospital Ocean Road Branch
11 Imalaseko Supermarket Posta – Pamba Street Posta Branch
12 Koli Finance Posta – J Mall/Habour View Tower/Samora Street J Mall Branch
13 Puma Petrol Station Kisutu – Jamuhuri Street Kitumbini Branch
14 Bahamadi Shop K/koo – Living stone/Agrey Street Opposite Bakhressa Depot
15 Bahamadi Shop K/koo – Mahiwa/Living Stone Street Nearby Kariakoo Bazar Bulding
16 Habibu Shop K/koo – Living stone/Pemba Street Opposite Green Bureau Change
17 Crown and Beauty Shop Mlimani City In Mlimani City Mall
18 Big Bon Sinza Mori At the Big Bon Petrol Station
19 C – Park Cub Kinindoni B Kinondoni B nearby Bus Stop
20 Baby Face Internet Café Mwananyamala (A) Near bus stop of Mwannyamala A
21 Treenaz G.Supplies Kawe – Mlalakuwa Street Opposite EFM Radio
22 Jukas Shop Africa Sana Opposite Africana Shop near the Africana Market
23 Puma Petrol Station Mbezi Bech Branch Between Interchick and Tank Bovu Bus Stops
24 Petro Fuel Station Tegeta Branch Near Azania Bus Stop
25 Swai Shop Ubungo Riverside At kibangu Bus stop
28 Virus Internet Café Magomeni – Magomeni Mapipa Nearby Mapipa Bus Stop
29 Bakari Shop Magomeni -Mwembe Chai Neaby Bus Stop Opposite Mosque
30 Twaha Shop Magomei – Kagera Nearby Old Kagera Bus Stop
31 Eshanaa Classic Ware Magomeni – Kagera Opposite Oil Com Petrol Station
32 Elvis Digital & Network Mbezi Louis Dealer of DSTV opposite Old Bus Stop
33 Mohamed Shop Mbagala Kongowe Nearest to the Bus Stop of Tua Ngoma
34 Merseytel Shop Mbagala Rangi Zakiem Opposite Darlive Pub
35 Kipanga Stationery Mtoni kwa Aziz Ally Nearby Aljazira Supermarket
36 Khadija Shop Mtoni kwa Aziz Ally Nearest to the Mtoni kwa Aziz Ally Bus stop
37 Olerai Tigo Super Agent Mtoni kwa Aziz Ally Nearest to the Halali Restaurant
38 Amiri Shop Kigamboni Ferry Nearest to the Ferry Station
39 Erick Shop Kigamboni Ferry Nearest to the Ferry Station
40 Ramadhani Shop Tandika Tandika Bus Stop

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA