Posts

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI, DECEMBER 31

Image

NEMC yakataza hoteli kutoza fedha wananchi wanaobarizi 'beach'

BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), limewataka wawekezaji wa hoteli zilizopo pembezoni mwa bahari kuacha kuwatoza wananchi fedha za kiingilio wanapokwenda katika fukwe hizo kupunga upepo au kuogelea. Tamko hilo limekuja kutokana na baadhi ya hoteli katika Jiji la Dar es Salaam kubainika kutoza fedha kuanzia Sh 10,000 hadi 40,000 kwa mtu mmoja kama gharama za kuogelea. Uchunguzi uliofanywa na MTANZANIA umebaini kuwa wamiliki wa hoteli hizo wamekuwa wakifanya hivyo katika sikukuu mbalimbali na zile za mwisho wa mwaka, jambo ambalo limekuwa likileta kero kwa jamii. Akizungumzia suala hilo Mwanasheria wa NEMC, Manchari Heche, alisema kwa mujibu wa sheria, fukwe zote ni mali ya umma, hivyo wananchi hawatakiwi kutozwa fedha wakati wanapokwenda kutembea au kuogelea. “Kifungu cha 57 cha sheria ya mazingira kimeweka ukomo wa mpaka wa kila kiwanja kilichopo karibu na ufukwe. “Beach (fukwe) zote ni mali ya umma kwa sababu kuna mipaka yake, hivyo kitendo cha kuwatoza w

KATUNI YA LEO.

Image

Kampuni za simu zatozwa faini; Wavietnam wa Halotel wakamatwa

Image
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye ulemavu), Bibi. Jenista Mhagama (Mb), akifuatilia maelezo ya wajumbe wa kikosi Maalum cha kukagua vibali vya Ajira za Wageni (hawapo pichani) wakati alipokutana nao Jijini Dar es Salaam tarehe 29 Desemba, 2015, (katikati) ni Naibu Waziri (Kazi, Ajira na Vijana), Anthony Mavunde na Katibu Mkuu (kazi na Ajira), Eric Shitindi. NAIBU Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde amebaini kuwepo kwa wafanyakazi wa kigeni, walioletwa na kampuni za simu za mkononi kufanya kazi zinazoweza kufanywa na Watanzania ikiwemo kufunga meza na viti vya kukalia. Aidha, amebaini kuwepo kwa baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya simu ya Halotel, raia wa Vietnam, ambao wanaishi nchini bila kibali cha kazi wala cha kuishi. Mavunde aliyabaini hayo jana wakati alipofanya ziara ya kukagua vibali vya ajira kwa wageni, baada ya tangazo lililotolewa na Waziri wa Ofisi ya Waziri Mk

Prof. Ndalichako ataja atakakoanzia ili kufufua kiwango cha elimu

Image
Prof. Ndalichako (wa kwanza kushoto, nyuma ya Katibu Mkuu Kiongozi) katika picha ya pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Katibu Mkuu Wa Kiongozi (walioketi) na Mawaziri (wote waliosimama) baada ya kuwapisha Ikulu jijini Dar es salaam Desemba 28, 2015.  WAZIRI wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako, amesema atafuatilia shule za Serikali ili kujua sababu za kufanya vibaya katika mitihani yao. Prof. Ndalichako ambaye aliwahi kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani (NECTA), amesema hayo juzi baada ya kuapishwa na Rais John Magufuli, kushika wadhifa huo. “Kwa kuwa lengo langu ni kuona elimu bora inatolewa, nitafuatilia kujua sababu ya shule maalumu za Serikali kushuka kiwango chake katika ufaulu wa mitihani,”  Kwa mujibu wa Prof. Ndalichako, shule hizo za Serikali hasa za vipaji maalum, ndizo awali kila mwanafunzi alipenda kwenda kusoma tofau

UFISADI MWINGINE WAIBULIWA BANDARINI DAR

Image
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa Serikali imepoteza jumla ya Sh. bilioni 48.47 baada ya makontena 11,884 na magari 2,019 kupitishwa badarini Dar es Salaam bila kulipiwa kodi. Hata hivyo, jumla ya watu saba wanashikiliwa na wengine nane wanatafutwa na Jeshi la Polisi kwa kuhusishwa na ukwepaji kodi huo uliolikosesha taifa mapato. Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema ufisadi huo umebainika baada ya serikali kuzifanyia ukaguzi bandari zote za nchi kavu (ICDs) jijini Dar es Salaam. Akifafanua, Waziri Mbarawa amesema makontena hayo 11,884 yalikuwa na thamani ya Sh. bilioni 47.4 wakati magari gari 2019 zenye thamani ya Sh. bilioni 1.07 yalitolewa bandarini pasipo kulipiwa tozo.

MAGAZETI YA LEO JUMATANO, DECEMBER 30

Image

CUF WATOA TAMKO ZANZIBAR

Image
Kaimu Mkurugenzi wa habari, uenezi na mawasiliano kwa umma Ismail Jussa. Kufuatia taarifa iliyotolewa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho iliyokutana Zanzibar juzi, tarehe 27 Desemba, 2015, waandishi wengi wa habari wametupigia simu wakitaka kujua Chama Cha Wananchi (CUF) kimepokea vipi taarifa ile. Vikao vya CCM ni vikao vya CCM. Si kawaida yetu kutolea taarifa maamuzi ya vikao vya vyama vyengine. Hata hivyo, tunaelewa ni kwa nini kumekuwepo na shauku ya kusikia CUF inasema nini kwa sababu yale yaliyokuwemo kwenye taarifa hiyo yaligusia pia mazungumzo yanayofanyika Ikulu Zanzibar yanayolenga kupata ufumbuzi wa mgogoro wa uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Oktoba, 2015. Baada ya kuipitia taarifa ya CCM na mengine yaliyoelezwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Zanzibar wakati akitoa ufafanuzi wa yale yaliyomo kwenye taarifa hiyo, CUF tunapenda kuwaeleza Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla haya yafuatayo: