UFISADI MWINGINE WAIBULIWA BANDARINI DAR
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa
Serikali imepoteza jumla ya Sh. bilioni 48.47 baada ya makontena 11,884 na magari 2,019 kupitishwa badarini Dar es Salaam bila kulipiwa kodi.
Hata hivyo, jumla ya watu saba wanashikiliwa na wengine nane wanatafutwa na Jeshi la Polisi kwa kuhusishwa na ukwepaji kodi huo uliolikosesha taifa mapato.
Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema ufisadi huo umebainika baada ya serikali kuzifanyia ukaguzi bandari zote za nchi kavu (ICDs) jijini Dar es Salaam.
Akifafanua, Waziri Mbarawa amesema makontena hayo 11,884 yalikuwa na thamani ya Sh. bilioni 47.4 wakati magari gari 2019 zenye thamani ya Sh. bilioni 1.07 yalitolewa bandarini pasipo kulipiwa tozo.
Comments
Post a Comment