Subi Nukta 1/12/2016 10:23:00 PM No Comment Mheshimiwa Ummy Mwalimu akizungumza na Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Peramiho, Dk Venance Mushi, alipotembelea hospitali hiyo SERIKALI imesema itapanga mgawanyo maalumu ili mikoa yote iweze kunufaika na huduma za Madaktari na Madaktari bingwa na kutatua kero za wananchi wanazopata za kufunga safari ndefu kuhangaikia huduma za wataalamu hao. Aidha itaendelea kushughulikia suala la kuboresha mazingira ya kazi kwa Madaktari na watumishi wa Sekta ya Afya kwa ujumla ikiwa ni pamoja na maslahi yao ili kuwafanya wahamasike kufanya kazi hapa nyumbani badala ya kwenda kufuata maslahi makubwa nje ya nchi. Kauli hiyo ya serikali imetolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na watoto Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa huduma za madaktari bingwa mkoani Ruvuma jana Alisema Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Daktari John Magufuli, imedhamiria kukabiliana na upungufu wa Madaktari kwa kuanzisha utaratibu maalumu