Posts

MGODI WA BUZWAGI WAPONGEZWA KWA KUZINGATIA SHERIA ZA MAZINGIRA

Image
Meneja wa kinu cha kuchenjua dhahabu wa Mgodi wa Buzwagi Festo Shayo (wa kwanza kulia) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais anaeshughulikia mazingira na Muungano, Luhaga Mpina namna mgodi wake unavyohifadhi maji yaliyotumika kusafishia dhahabu. Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira na Muungano Luaga Mpina (wa kwanza kushoto), akisikiliza maelezo ya Afisa Mazingira wa Mgodi wa Buzwagi bwana Frank Ngoroma (wa kwanza mkono wa kulia), aliyesimama katikati ni meneja mkuu wa mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo. Mh Luhaga Mpina akisisitiza jambo wakati wa ziara hiyo katika eneo la kituo cha Uthibiti wa taka mbalimbali mgodini hapo. Naibu Waziri pamoja na wataalamu wake wakikagua moja ya maeneo ambayo NEMC yalitoa ushauri kuwa yafanyiwe kazi katika ziara zao, ambapo wakati wa ziara hii utekelezwaji wake ulikutwa umeisha kamilika kama walivyokuwa wameelekezwa Mmoja wa maafisa wa mazingira aliyekuwa ameandamana na naibu Waziri akiuliza jamb

MAGAZETI YA LEO JUMATATU, JANUARY 18

Image

SERIKALI YATOA TAMKO KUHUSU TIBA ASILI NA TIBA MBADALA

Image
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akitoa uamuzi wa Serikali kuhusu Serikali kuhusu Tiba Asili  na Tiba Mbadala katika mkutano wa  waandishi  ulifanyika jana kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo. kushoto ni  Naibu Waziri wa Wizara hiyo, DK. Hamis Kigwangalla wakifuatilia tukio hilo. Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigangwalla akifafanua jambo kuhusu uamuzi wa  Serikali kuhusu Tiba Asili  na TibaMbadala katika mkutano wa  waandishi  ulifanyika jana kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo. kushoto ni  Waziri wa Wizara hiyo, Ummy Mwalimu.

Taarifa ya hatua ya TMAA dhidi ya waliotorosha, na biashara haramu ya madini

Image
UDHIBITI WA UTOROSHAJI NA BIASHARA HARAMU YA MADINI  Moja ya majukumu ya Wakala wa Ukaguzi wa madini Tanzania (TMAA) ni kufuatilia na kuzuia utoroshaji/magendo na biashara ya madini unaopelekea ukwepaji wa ulipaji mrabaha kwa kushirikiana na taasisi nyingine husika za Serikali zikiwemo Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), Jeshi la Polisi, Idara ya Usalama wa Taifa, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Idara ya Uhamiaji.  Taarifa za matukio ya udhibiti wa utoroshaji na biashara haramu ya madini zilizopo zinaonesha kuwa katika kipindi cha kuanzia mwezi Julai 2015 mpaka Januari 13, 2016 kulikuwepo na jumla ya matukio 14 ya utoroshaji wa madini ambapo madini yenye thamani ya Dola za Marekani 1,474,194 milioni (zaidi ya Shilingi bilioni 3,235,856,181) yalikamatwa na wakaguzi wa Wakala kupitia Madawati ya Ukaguzi yaliyopo katika viwanja vya ndege vya Dar es Salaam (JNIA), Kilimanjaro (KIA) na Mwanza.  Katika matukio ya hivi karibuni ya ukamataji wa madini katika viwanja vya ndege, madi