Posts

WAZIRI WA AFYA MH. UMMY MWALIMU NA NAIBU WAKE WATEMBELEA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI KUKAGUA

Image
  Dk.Stanslaus Ntiyakunze (aliyenyoosha mkono) akiwaonyesha mawaziri namna jengo linavyokarabatiwa ikiwemo miundombinu yake inavyotakiwa kuwa pindi litakapokamilika ikiwemo suala la mfumo wa maji safi na maji taka. Kuliwa kwake ni Naibu Waziri wa Afya Dk Hamisi Kigwangalla wengine Kaimu Mkurugenzi wa hospitali hiyo ya Muhimbili, Prof. Laurance Masaru (kushoto) na Waziri wa Afya, Mh. Ummy Mwalimu (katikati). Mawaziri wa Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli wameendelea kufanya kile ambacho wananchi wanataka ikiwemo suala la kutumikia wananchi ambapo mapema leo, Februari 17, Mawaziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu na Naibu wake, Dk. Hamisi Kigwangalla wameweza kutembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa lengo la kukagua majengo likiwemo lile aliloagiza Rais kuwa litumike kuwa wodi ya akina mama. Mawaziri hao wamefika Hospitali hiyo ya Taifa majira ya mchana na kisha kupokelewa na wenyeji wao akiwemo Kaimu

Polisi yazima ghasia iliyozuka kati ya Wamasai na Watatoga wa Simanjiro na Kondoa

Image
Info Post Subi Nukta 2/18/2016 12:01:00 AM No Comment

TTCL yakanusha taarifa za mfumo wake wa mawasiliano kuingiliwa na kudukuliwa

Image
Meneja wa Kitengo cha Usalama Mifumo ya Mawasiliano ya TTCL, Lina Rujweka akifafanua jambo kwenye mkutano na vyombo vya habari leo. KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) imekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni kuwa mfumo wa mawasiliano wa kampuni hiyo umeingiliwa na wadukuzi. Taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam na Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo, Nicodemus Thomas Mushi alisema taarifa zinazotolewa si za kweli hivyo kuwataka wateja wao wazipuuze. “...Tunapenda kuwathibithia Wateja wetu wote wa ndani na nje ya nchi, wadau wetu na Umma kwa ujumla kwamba, taarifa hizi si sahihi, na kwamba mifumo yetu ya Mawasiliano ya TTCL ipo salama, huduma zetu zote zipo thabiti na mpaka sasa tunapotoa taarifa hii, hakuna uhalifu wowote uliofanyika kwa sisi wenyewe kama Kampuni wala kwa mteja wetu yeyote,” alisema Thomas Mushi. Aidha, tunapenda kuwathibitishia kuwa, taarifa za Wateja wetu wote ikiwemo Serikali , Idara, Wakala na Taasisi za Umma, Taasisi za fedha, M

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI, FEBRUARY 18

Image

MKE WA RAIS MAMA JANETH MAGUFULI AAGWA RASMI SHULE YA MSINGI MBUYUNI

Image
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa ameketi kwenye meza yake katika ofisi ya waalimu katika shule ya Msingi ya Mbuyuni jijini Dar es salaam wakati wa sherehe fupi ya kuwaaga rasmi walimu wenzake na wanafunzi wa shule hiyo ambayo ana historia nayo ndefu sana kwani ndipo yeye mwenyewe aliposomea elimu ya msingi toka darasa la kwanza hadi la saba kabla hajarudi tena hapo kama mwalimu na kufanya kazi kwa miaka 17 mfululizo.

TAARIFA KUTOKA BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA KUHUSU MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2015

Image
Baraza la Mitihani la Tanzania limekuwa likipigiwa simu na watu mbalimbali wakiomba ufafanuzi kuhusu taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi imetangaza kuwa matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) 2015 yamezuiwa kwa muda hadi tarehe 08/03/2016.  Baraza la Mitihani la Tanzania linapenda kuwajulisha watahiniwa na umma kwa ujumla kuwa taarifa hizo ni za UONGO na zinalenga kupotosha umma na kuleta taharuki. Hivyo, Baraza linaomba umma kuzipuuza taarifa hizo kwa kuwa Wizara haijasitisha utoaji wa matokeo hayo. Matokeo yatatangazwa mara tu mchakato utakapokamilika.  Imetolewa na,  AFISA HABARI NA UHUSIANO  TAARIFA NECTA