Posts

RC PAUL MAKONDA AZUNGUMZA NA WENYEVITI NA MAOFISA WATENDAJI WA JIJI LA DAR

Image
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akizungumza na wenyeviti na maofisa watendaji wa jiji la Dar es Salaam jana asubuhi kuhusu mambo mbalimbali hasa suala la usafi wa mazingira.  Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando akiongoza mkutano huo.  Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akizungumza katika mkutano huo.  Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema akizungumza katika mkutano huo.  Mwakilishi wa Taasisi ya Wakala wa Upimaji Ardhi Tanzania, Linus Kinyondo akizungumzia suala zima la ujenzi wa nyumba kwa kuzingatia mipango miji ili kutunza mazingira.  Wenyeviti na maofisa watendaji wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda (hayupo pichani)

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI, MACHI 20

Image

DK. AYUB RIOBA CHACHA MKURUGENZI MKUU TBC

Image

Watakaokutwa wakicheza "pool table" kabla ya saa 10 kutozwa faini 300,000/=

Image
Wapenzi wa mchezo wa  pool table  nchini, watalazimika kusubiri hadi saa 10 jioni kucheza mchezo huo au kukubali kutozwa faini isiyopungua Sh300,000 wakikutwa wanacheza kabla ya muda uliopangwa.  Mkurugenzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Abbas Tarimba amesema wametayarisha barua zitakazotumwa kwa wakuu wa mikoa ili kuwasaidia kuelekeza wananchi kuhusu kanuni, sheria na taratibu za mchezo huo.  Alisema barua hizo pamoja na matangazo yatakayotoka katika vyombo vya habari, vitatoa mwongozo wa muda wa kuanza mchezo huo ambao utakuwa ni saa 10.00 jioni na kumaliza saa 5.00 usiku kwa siku za kazi, huku siku za mapumziko utaanza saa 8.00 mchana na kumalizika saa 6.00 usiku.  Tarimba alisema Sheria ya Michezo ya Kubahatisha (Gaming Act), kifungu cha 52 katika kifungu kidogo cha kwanza sura ya 42, inaeleza asiye na kibali cha kuchezesha au atakayekiuka kanuni za mchezo huo, atashtakiwa na akikutwa na hatia atalazimika kulipa faini isiyopungua Sh300,000 au kifungo kisichopungua miezi m

Wachina wamehukumiwa jela miaka 30,waliokamatwa wakiwa na vipusa vya ndovu

Image
Kutoka kulia ni na Xu Fujie na Huang Jing Raia wawili wa China wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 au kulipa zaidi ya sh. bilioni 54 kila mmoja kwa kukutwa na hatia ya makosa mawili. Washitakiwa hao katika kosa la kwanza walikutwa na hatia ya kukutwa na nyara za serikali, vipande 706 vya vipusa vya tembo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni tano wakati kosa la pili ni la kushawishi kwa kutoa rushwa kwa askari kiasi cha shilingi milioni 30/=. Washitakiwa hao Huang Jing pamoja na Xu Fujie wameanza kutumikia kifungo hicho leo baada ya kushindwa kulipa faini. Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Kisutu, Cyprian Mkeha alitoa hukumu kwa watuhumiwa hao na kusema wanaweza kukata rufaa katika Makahakama Kuu. Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi aliomba mahakama iwape adhabu kali kutokana na kosa waliolifanya na kudai kuwa kutokana na kukamatwa kwao vitendo vya uhalifu kwa wanyamapori vimepungua. Wakili upande wa washitakiwa, Nehemia Mkoko aliomba mahakama kuwaonea hurum

Polisi yakamata 2 watuhumiwa wa kusambaza dawa za kulevya Afrika Mashariki

Info Po Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salam, Kamishna Simon Siro amesema kuwa Jeshi la Polisi mkoani Dar es Salaam, limefanikiwa kumkamata Hussein Khalil anayetuhumiwa kuwa msambazaji wa dawa za kulevya jijini Dar es Salaam na katika miji ya nchi za Afrika Mashariki. Mtuhumiwa huyo alikuwa akitafutwa kwa muda mrefu kabla ya kutiwa mbaroni baada ya kupatikana kwa taarifa za siri kutoka kwa raia, ambapo aliwekewa mtego baada ya kukamatwa kwa mshirika wake aliyetambuliwa kwa jina la Benson Charles Muro, ambaye alikutwa na "mzigo" wa heroin kilogramu moja kwenye gari lenye namba za usajili T407BMM aina ya Toyota Hilux, pickup, huko Mbezi Beach jijini Dar es Salaam. "Baada ya kumtilia mashaka tulipomkamata, tukamkuta na hayo madawa ya kulevya. Alipohojiwa akasema, ' jamani mimi ni kweli nimetumwa na bosi wangu .' Sasa kwa sababu hili jina la Hussein Mohammed Halili linafahamika, tumamwuliza, yuko wapi?, akasema ' yupo kwenye kituo cha mafuta

TCRA YAPELEKA BIL. 40.6 KATIKA MFUKO WA SERIKALI (HAZINA)

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema mpaka sasa mamlaka imepeleka fedha kwenye mfuko wa serikali (hazina) kiasi cha Sh. 40,656,865,447.03 ambazo nimakusanyo ya kuanzia Oktoba, 2013 hadi Agosti, 2015. Hayo yamesemwa Dar es salaam, wakati wa mkutano wa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za mamlaka ya mawasiliano, Mkurugezi mkuu wa Mawasiliano Tanzania, Dk.Ally Simba. Pia alisema kumesaidia kuweza kudhibiti mawasiliano ya ulaghai na hivyo kuweza kudhibiti vitendo viovu vinavyofanyika kupitia njia hiyo na kuimarisha usalama nchini. “Kifungu cha 6(1) kinaelezea kanuni za TTMS zinaitaka mamlaka ya mawasiliano kuwasilisha asilimia 28 ya mapato yatokanayo na mtambo wa kuhakiki mawasiliano ya simu kutoka nje ya nchi katika mfuko mkuu wa serikali,” alisema Simba. Dk.Simba alisema kuwa mfumo wa kusimamia mawasiliano TTMS umesaidia kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa sheria na kanuni zilizopo katika kudhibiti sekta ya mawasiliano. Aidha alisema mamlaka imefanikiwa kuf