Polisi yakamata 2 watuhumiwa wa kusambaza dawa za kulevya Afrika Mashariki

Info Po
Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salam, Kamishna Simon Siro amesema kuwa Jeshi la Polisi mkoani Dar es Salaam, limefanikiwa kumkamata Hussein Khalil anayetuhumiwa kuwa msambazaji wa dawa za kulevya jijini Dar es Salaam na katika miji ya nchi za Afrika Mashariki.

Mtuhumiwa huyo alikuwa akitafutwa kwa muda mrefu kabla ya kutiwa mbaroni baada ya kupatikana kwa taarifa za siri kutoka kwa raia, ambapo aliwekewa mtego baada ya kukamatwa kwa mshirika wake aliyetambuliwa kwa jina la Benson Charles Muro, ambaye alikutwa na "mzigo" wa heroin kilogramu moja kwenye gari lenye namba za usajili T407BMM aina ya Toyota Hilux, pickup, huko Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.

"Baada ya kumtilia mashaka tulipomkamata, tukamkuta na hayo madawa ya kulevya. Alipohojiwa akasema, 'jamani mimi ni kweli nimetumwa na bosi wangu.'
Sasa kwa sababu hili jina la Hussein Mohammed Halili linafahamika, tumamwuliza, yuko wapi?, akasema 'yupo kwenye kituo cha mafuta ananisubiri''.
Kwa hiyo tulipokwenda, tukamkuta. Alipoiona ile pickup akakimbia kuja kuchukua mzigo, tukawa tumemkamata," amesema Kamanda Siro.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA