Posts

Getrude Clement (Youth Representative from Tanzania) High-level Signature Ceremony for the Paris Agreement

Image

Waziri Muhongo na ujumbe wake warejea nchini baada ya makubaliano ya mafuta ghafi ya Uganda kutumia bomba la Tanzania

Image
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kati) akiwasili jijini Dar es salaam , akitokea Jijini Kampala alikoenda kukamilisha dili la bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanga, alioongozana nao ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa (kulia) pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dk. Juliana Pallangyo. Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, akionyesha kwa wanahabari, mpango wa ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka nchini Uganda mpaka Jijini Tanga, mara tu baada ya kuwasili nchini akitokea jijini Kampala. Mbali na kunufaika kwa Watanzania kupitia Mpango huo, pia utazinufaisha nchi nyingine za Afrika Mashariki na Kati. Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa (kulia), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dk. Juliana Pallangyo (wa pili kulia) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio walipokuwa wakimsubiria Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sos

Watumishi hewa Kilimanjaro: Hai yataja waliofutwa kazi kwa kukopa, kununua 'dawa hewa", kuiba malipo ya "overtime"

MSAKO ulioanzishwa na Rais John Magufuli wa kutokomeza tatizo la wafanyakazi hewa katika utumishi wa umma, umeendelea kuibua mazito, ambapo mkoani Kilimanjaro, Benki ya CRDB imejikuta ikitoa mkopo kwa waliokuwa wafanyakazi hewa.  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai, Helga Mchomvu aliyasema hayo akidai kuwa, yamegundulika baada ya Serikali kuunda kamati za uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu wa zaidi ya Sh milioni 500 katika halmashauri hiyo.  Kabla ya kuibuka kwa kisa hicho kinachoonesha namna wafanyakazi hewa alivyokuwa wakiibia nchi, hivi karibuni mkoani Singida, Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Imani Nyamangaro, alipandishwa kizimbani akidaiwa kujilipa mishahara ya wastaafu 57, yenye thamani ya Sh milioni 29.4.  Mbali na mhasibu huyo, Rais Magufuli alipokuwa mapumziko kijijini kwake Mlimani, katika Wilaya ya Chato mkoani Geita, alieleza kisa kingine kilichoshitua jamii kuwa katika Mamlaka ya Mapato (TRA), kulikuwa na mtumishi mmoja ambaye alikuwa akilipwa mi

HISTORIA YA PAPA WEMBA

Image
Habari kuwa mmoja wa vigogo wa muziki wa kiafrika Papa Wemba ametutangulia mbele ya haki imepokewa kwa mshtuko mkubwa na mashabiki wake kote duniani. Video inayosambazwa katika mitandao ya kijamii inamuonesha Papa Wemba akiendelea na kazi yake anayoifahamu zaidi ya uimbaji kisha anaonekana akianguka ghafla jukwaani. Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba 1949-2016. Wanabendi wake waliokuwa jukwaani naye huko Abidjan katika tamasha la muziki la #FEMUA wanaendelea kupiga densi tu kabla ya mmoja wao kukimbia kumuokoa baada ya kuona kasalia chini kwa sekunde kadhaa akiwa anatetemeka kisha akazirai. Shoo hiyo ya Papa Wemba ilikuwa moja katika mji mkuu wa Ivory Coast Abidjan. Msemaji wake Henry Christmas Mbuta Vokia, ameiambia Radio Okapi kuwa ''Marehemu Papa Wemba alikuwa ameingia muda mchache tu jukwaani kisha akacheza wimbo wa kwanza, mashabiki wakamuomba awaimbie tena wimbo mwengine akakubali. lakini dakika chache tu baada ya kuanza kupiga wimbo wa ke wa tatu Papa Wem

TRA "tulishamfukuza kazi" mwajiriwa aliyethibitisha kujilipa mishahara 17

Mfayakazi wa Mamlaka ya Mapato Nchini aliyetuhumiwa na Rais John Magufuli mwezi uliopita kujilipa mishahara 17 ya watumishi hewa, hayupo kwenye ajira ya TRA kwa siku nyingi zilizopita, imefahamika.  Habari kutoka ndani ya Mamlaka hiyo zimesema kuwa mfanyakazi huyo alikuwa ni wa Idara ya Uhasibu ya TRA lakini alishafukuzwa kazi siku nyingi zilizopita.  Chanzo cha kuaminika kutoka Makao Makuu ya TRA kimeiambia Nipashe kuwa mfanyakazi huyo alifukuzwa kazi baada ya kubainika kujilipa mishahara hiyo katika akaunti yake.  Chanzo chetu cha habari ambacho hakikupenda kutajwa jina gazetini kwa sababu si msemaji wa mamlaka, kilisema mfanyakazi huyo baada ya kuhojiwa alikiri kujilipa mishahara hiyo.  Ndipo alipochukuliwa hatua za kufukuzwa kazi pamoja na kufikishwa Mahakamani, kilisema chanzo hicho. “Huyu mfanyakazi alikuwa Idara ya Uhasibu... ni kweli alijilipa mishahara hiyo na baada ya kuhojiwa alikiri ndipo tukamfukuza kazi na kumpeleka mahakamani,” chanzo hicho kilieleza.  “(Lakini)

Taarifa ya habari ChannelTEN, Aprili 24, 2016

Image

MAGAZETI YA LEO JUMATATU, APRIL 25

Image