Waziri Muhongo na ujumbe wake warejea nchini baada ya makubaliano ya mafuta ghafi ya Uganda kutumia bomba la Tanzania

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kati) akiwasili jijini Dar es salaam , akitokea Jijini Kampala alikoenda kukamilisha dili la bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanga, alioongozana nao ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa (kulia) pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dk. Juliana Pallangyo.


Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, akionyesha kwa wanahabari, mpango wa ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka nchini Uganda mpaka Jijini Tanga, mara tu baada ya kuwasili nchini akitokea jijini Kampala. Mbali na kunufaika kwa Watanzania kupitia Mpango huo, pia utazinufaisha nchi nyingine za Afrika Mashariki na Kati.


Comments
Post a Comment