WATAKA UWANJA WA NDEGE MWANZA UJENGWE KISASA ILI KUINUA SEKTA YA UTALII
Na Tiganya Vincent-MAELEZO_Dodoma Baadhi ya Wabunge wanaotoka Kanda ya Ziwa wameomba Wizara ya Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano kujenga Uwanja wa Ndege wa Mwanza kwa kiwango cha Kimataifa ili kuimarisha sekta ya Utalii na usafiri wa anga katika kanda ya Ziwa. Walisema kuwa hatua itasaidia watalii wanaokuja nchini kushuka moja kwa moja mkoani Mwanza na kisha kuelekea katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na maeneo mengine ya vivutio vya hapa nchini bila kupitia nchi jirani. Kauli hiyo imetolewa jana na Wabunge Dkt.Raphael Chegeni na Mhe. Ezekeil Maige wakati wakichangia hotuba kuhusu utekelezaji wa bajeti ya Wizara ya Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka ujao wa fedha. Mhe. Dkt.Chegeni alisema kuwa Uwanja wa Ndege wa Mwanza ni muhimu ukajengwa kwa viwango vya Kimataifa ili uweze kuruhusu ndege mbalimbali kubwa na ndogo kuweza kutua bila tatizo. Alisema kuwa hatua hiyo itasaidia kuunganisha Mkoa wa Mwanza na nchi jirani za Rwanda, Uganda na Burundi na hivyo kuruhusu