Posts

Magazeti ya Leo Jumapili

Image

Obama aelekea katika ziara Vietnam na Japan

Image
Rais Obama (kulia)akisalimiana na kiongozi wa chama cha kikomunist cha Vietnam Nguyen Phu Trong(kushoto) Rais wa Marekani Barack Obama ameondoka jana Jumamosi (21.05.2016)kwenda katika ziara nchini Vietnam na Japan ambayo itajumuisha ziara ya kwanza mjini Hiroshima kwa rais wa Maarekani aliyeko madarakani. Obama amesafiri kwa ndege rasmi ya rais ya Air Force One katika mkondo wa kwanza wa ziara hiyo, ambayo itamalizika kwa kusimama kwa muda kutia mafuta katika kituo cha kijeshi cha Elmendrf katika eneo la Anchorage , jimboni Alaska. Ziara ya kumi ya rais Obama katika bara la Asia ina lengo la kufunga kurasa mbaya katika vita viwili vya karne ya 20 katika eneo hilo ambalo analiona kuwa muhimu katika hali ya baadaye ya Marekani. Ziara hiyo itaanzia Hanoi, ambako Obama atasisitiza kuimarisha uhusiano na nchi hiyo inayojitokeza kwa kasi na kwa nguvu kiuchumi, lakini ni nchi ambayo , kwa Wamarekani wengi , inabakia kwa maneno kuwa nchi ya ma

HABARI ZILIZOPO KWENYE MAGAZETI YA LEO MAY 20

Image
TANZANIA KENYA UGANDA

WATAKA UWANJA WA NDEGE MWANZA UJENGWE KISASA ILI KUINUA SEKTA YA UTALII

Image
Na Tiganya Vincent-MAELEZO_Dodoma Baadhi ya Wabunge wanaotoka Kanda ya Ziwa wameomba Wizara ya Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano kujenga Uwanja wa Ndege wa Mwanza kwa kiwango cha Kimataifa ili kuimarisha sekta ya Utalii na usafiri wa anga katika kanda ya Ziwa. Walisema kuwa hatua itasaidia watalii wanaokuja nchini kushuka moja kwa moja mkoani Mwanza na kisha kuelekea katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na maeneo mengine ya vivutio vya hapa nchini bila kupitia nchi jirani. Kauli hiyo imetolewa jana na Wabunge Dkt.Raphael Chegeni  na Mhe. Ezekeil Maige wakati wakichangia hotuba kuhusu utekelezaji wa bajeti ya Wizara ya Ujenzi ,Uchukuzi  na Mawasiliano kwa mwaka ujao wa fedha. Mhe. Dkt.Chegeni alisema kuwa Uwanja wa Ndege wa Mwanza ni muhimu ukajengwa kwa viwango vya Kimataifa ili uweze kuruhusu ndege mbalimbali kubwa na ndogo kuweza kutua bila tatizo. Alisema kuwa hatua hiyo itasaidia kuunganisha Mkoa wa Mwanza na nchi jirani za Rwanda, Uganda na Burundi na hivyo kuruhusu

MKWASA ATAJA KIKOSI CHA NYOTA 27

Image
Kocha Mkuu wa timu ya Soka ya Tanzania, Charles Boniface Mkwasa ameita kikosi cha wachezaji 27 watakaounda Taifa Stars ambacho kinajiandaa kucheza Misri Juni 4, 2016 katika mchezo wa kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON-2017). Mkwasa maarufu kama Master, alitangaza kikosi cha timu hiyo Jana Mei 18, 2016 mbele ya Kocha Msaidizi, Hemed Morocco na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam. Kabla ya kuiva Misri, kikosi hicho kitafunga safari hadi Kenya kucheza na Harambee Stars katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa ambao wenyeji wameuombea Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kwamba utambulike na kuingia kwenye rekodi za kimataifa ikiwa ni pamoja na kuingia kwenye mchakato wa kupima viwango vya soka. Katika kikosi hicho, Mkwasa amemuita beki Mlinzi mahiri wa Young Africans, Nadir Haroub maarufu kama Cannavaro huku akimwacha beki mwingine wa Young Africa