Obama aelekea katika ziara Vietnam na Japan
Rais Obama (kulia)akisalimiana na kiongozi wa chama cha kikomunist cha Vietnam Nguyen Phu Trong(kushoto)
Rais wa
Marekani Barack Obama ameondoka jana Jumamosi (21.05.2016)kwenda katika
ziara nchini Vietnam na Japan ambayo itajumuisha ziara ya kwanza mjini
Hiroshima kwa rais wa Maarekani aliyeko madarakani.
Obama
amesafiri kwa ndege rasmi ya rais ya Air Force One katika mkondo wa
kwanza wa ziara hiyo, ambayo itamalizika kwa kusimama kwa muda kutia
mafuta katika kituo cha kijeshi cha Elmendrf katika eneo la Anchorage ,
jimboni Alaska.
Ziara ya
kumi ya rais Obama katika bara la Asia ina lengo la kufunga kurasa mbaya
katika vita viwili vya karne ya 20 katika eneo hilo ambalo analiona
kuwa muhimu katika hali ya baadaye ya Marekani.
Ziara
hiyo itaanzia Hanoi, ambako Obama atasisitiza kuimarisha uhusiano na
nchi hiyo inayojitokeza kwa kasi na kwa nguvu kiuchumi, lakini ni nchi
ambayo , kwa Wamarekani wengi , inabakia kwa maneno kuwa nchi ya mauaji
na upumbavu.
Suala kuu
la mazungumzo litakuwa kuondoa marufuku ya silaha iliyowekwa na
Marekani, alama iliyobakia katika vita ambavyo vilimalizika mwaka 1975.
Atakutana na rais, waziri mkuu, kiongozi wa bunge la taifa na kiongozi
mkuu wa nchi hiyo Nguyen Phu Trong, katibu mkuu wa chama cha kikomunist.
Mivutano ya kugombea maeneo ya habarini Trong na
Obama walikutana Julai mwaka jana, wakati kiongozi huyo wa Vietnam
alipopewa fursa adimu ya kukutana na rais wa Marekani katika ofisi kuu
ya rais ya Oval mjini Washington. Mivutano mikali kuhusiana na masuala
ya maeneo ya baharini kati ya Vietnam na jirani yake mkubwa China huenda
pia ikajadiliwa kwa kina.
Wanaotaka
vikwazo vya silaha viondolewe wanadai kwamba ni muhimu kuisaidia
Vietnam kuimarisha ulinzi wake wa pwani na kuimarisha jeshi lake dhidi
ya China.
Nchini
Japan , Obama atahudhuria mkutano wa kundi la mataifa ya G7 na kuweka
historia kwa kuwa rais wa kwanza wa Marekani aliyeko madarakani
kutembelea Hiroshima, ambako mwaka 1945 rais wa wakati huo wa Marekani
Harry Truman aliamuru kushambulia kwa bomu la kwanza la kinyuklia
duniani.
Ziara hiyo mjini Hiroshima imezusha hata hivyo mjadala juu ya iwapo uamuzi wa Truman ulikuwa wa haki.
Wamarekani
wengi wanaamini kwamba wakati bomu hilo liliuwa kiasi ya Wajapani
140,000, kuishambulia Hiroshima kwa bomu na kisha Nagasaki kumeepusha
uvamizi mkubwa zaidi wa ardhini wa japan.
Wahanga wa mashambulizi hayo ya bomu wametoa wito wa kuombwa msamaha , ambapo Ikulu ya marekani inasema haiko tayari kutoa.DW
Comments
Post a Comment