Posts

Taarifa ya habari ChannelTEN Juni 26, 2016

Image

Taarifa ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu kwa waombaji

Image
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Inapenda kutoa taarifa kwa Umma na wadau wake wote kuwa inatarajia kuanza kupokea maombi ya Mikopo kwa mwaka wa masomo 2016 /2017 kuanzia tarehe 27 Juni 2016 hadi tarehe 31 Julai 2016. Katika kipindi hicho waombaji wa mikopo watarajiwa wanapaswa kusoma mwongozo wa utoaji mikopo na ruzuku uliopo kwenye tovuti ya Bodi www.heslb.go.tz ili kufahamu sifa za mwombaji na taratibu kufuata kabla ya kuomba mikopo kwa njia ya mtandao. Utoaji wa Mikopo unaongozwa na Sheria ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya juu Na. 9 ya 2004 (kama ilivyorekebishwa) hususani vifungu vyake vya 16 na 17. Kwa taarifa hii, waombaji wote wa mikopo wanatakiwa kusoma mwongozo huo kabla ya kujaza maombi ya mikopo na wazingatie kuwa tarehe ya mwisho ya kuomba mikopo ni Julai 31, 2016. IMETOLEWA NA: KITENGO CHA HABARI, ELIMU NA MAWASILIANO BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU TAREHE 24 JUNI 2016.

[video] Hotuba ya Rais Magufuli wakati wa makabidhiano ripoti ya Uchaguzi Mkuu 2015

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (kushoto) akisalimiana na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya kuwasili katika Ukumbi wa Ikulu, kwa ajili ya makabidhiano ya taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wageni waalikwa (hawapo pichani) katika hafla ya Makabidhiano ya taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka 2015. Taarifa hiyo imekabidhiwa leo na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji Damian Lubuva kwa Mhe. Rais Magufuli, katika hafla iliyofanyika Ikulu, Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Viongozi Wakuu wastaafu wa Serikali, Viongozi wa Tume ya Uchaguzi Tanzania Bara na Zanzibar, Waheshimiwa Mawaziri na Viongozi Waandamizi wa Serikali, wengine ni Viongozi Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama, Waheshimiwa Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa wanaow

RAIS WA RWANDA PAUL KAGAME ZIARANI TANZANIA

Image
Rais Paul Kagame anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi jijini Dar es Salaam, nchini Tanzania Julai 1 kwa mwaliko wa mwenzake wa Tanzania Rais John Pombe Magufuli. Katika ziara hiyo Rais Paul Kagame atafungua mkutano wa kimataifa wa 40 wa wafanyabiashara, Dar es Salaam International Trade Fair (DITF) na kufanya mazungumzo yenye lengo la kuimarisha mahusiano baina ya nchi hizi mbili. Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Nje, Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Mahiga, rais wa Rwanda atafanya ziara ya kikazi nchini Tanzania baada ya kualikwa na mwenziye wa Tanzania, Rais John Magufuli. Wakati wa ziara hiyo, Bw Kagame na ujumbe wake wanatarajiwa kutia saini Mkataba wa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili (MoU), ambo ulikamilishwa na kamati ya pamoja ya wataalam kutoka nchi zote mbili. Nchi hizi mbili jirani, mwezi uliopita, zilikubaliana kuunda kamati ya pamoja ya utekelezaji (JIC) itakayofuatilia kwa karibu utekelezaji wa miradi muhi

MAGAZETI YA LEO IJUMAA, JUNE 24

Image

Kamishna Kova aagwa rasmi kustaafu kazi ya utumishi wa umma

Image
Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova akipunga mkono kwa Maofisa, wakaguzi, Askari na wageni mbalimbali waliohudhururia sherehe za kumuaga rasmi Jeshini baada ya kustaafu utumishi zilizoongozwa na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki katika Chuo cha Polisi Moshi. Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova akikagua gwaride maalumu lililoandaliwa kwa ajili yake wakati wa sherehe za kumuaga rasmi Jeshini baada ya kustaafu utumishi zilizoongozwa na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki katika Chuo cha Polisi Moshi Maofisa wa Polisi wakisukuma gari maalumu lililombeba Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi Suleiman Kova kutoka katika viwanja vya Chuo cha Polisi Moshi wakati wa sherehe za kumuaga rasmi Jeshini baada ya kustaafu utumishi zilizoongozwa na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki. Gari maalumu lililombeba Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi Suleiman Kova likipita katika ya gwaride ikiw

ELIMU KWA UMMA JUU YA MANUFAA YA MATUMIZI YA MAJINA YA KIKOA CHA DOT TZ (.TZ DOMAIN NAMES)

Image
Taarifa kwa umma kuhusu matumizi ya majina ya kikoa cha .tz TAARIFA KWA UMMA TOKA RAJISI YA DOT TZ YAH: ELIMU KWA UMMA JUU YA MANUFAA YA MATUMIZI YA MAJINA YA KIKOA CHA DOT TZ (.TZ DOMAIN NAMES) Tanzania Network Information Centre (tzNIC) au Rajisi ya dot tz ni kampuni inayoendesha na kusimamia rasilimali ya nchi (dot tz) kwa ajili mawasiliano kupitia mtandao wa Intaneti. tzNIC inapenda kuuarifu umma wa watanzania kuwa imetenga siku za Jumatatu (27 Juni 2016) na  Jumanne (28 Juni 2016) kutoa elimu kwa umma juu ya kazi zake, manufaa ya matumizi ya majina ya kikoa cha dot tz (.tz domain names) na namna bora ya kuhama kutoka matumizi ya majina mengine ya vikoa kama dot com na dot org kwenda kikoa cha dot tz. Katika kipindi hicho tzNIC pia itapokea maoni mbalimbali juu ya uboreshaji wa huduma zake na nini kifanyike ili watanzania wengi wasajili na kutumia majina ya kikoa cha dot tz kwa ajili ya biashara zao, huduma zao na matumizi binafsi. Tukio hili l

Magazeti ya Leo Alhamisi, June 23

Image