WANANCHI WA WILAYA YA UBUNGO WAKO MBIONI KUSOGEZEWA HUDUMA
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Boniface Jacob akisalimiana na Mkuu wa Wialaya ya Ubungo Mhe. Humphrey Polepole alipokaribishwa katika Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Kinondoni jana Jijini Dar es Salaam. Polepole amekaribishwa ili apate fursa ya kutambulishwa kwa Madiwani ambao kwa namna moja au nyingine atakuwa akifanya kazi nao kwa kuwa Wilaya yake imetokana na Manispaa hiyo. Frank Shija,MAELEZO Mchakato wa kukamilisha taratibu za kuanza rasmi kwa shughuli za kiutendaji kwa Ofisi za Mkuu wa wilaya na Manispaa ya Ubongo uhuko mbio kukamilika. Kauli hiyo imetolewa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kindondoni ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Ubungo Mhe. Boniface Jacob wakati wa Kikao cha Baraza la Madiwani jana jijini Dar es Salaam. Mhe. Jacob amesema kuwa amearifiwa kuwa taratibu za kugawa rasilimali zimekamilika kinachosubiriwa tu ni kukamilika kwa suala la upatikanaji wa majengo ya Ofisi ambayo nayo yako mbioni kupatikana. Jacob aliongeza kuwa kukamilika kwa m