Polisi Wakamata Vyeti Bandia, Leseni za Biashara na Silaha Dar

1.Kamishina wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Simon Sirro akiongea na wanahabari(hawapo pichani).
Kamishina wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Simon Sirro akiongea na wanahabari (hawapo pichani).
7.Akionesha bunduki iliyokamatwa.
Akionesha bunduki iliyokamatwa.
6...akiendelea kuonesha.
5.Kamanda Sirro akionesha vyeti bandia vya sekondari.
Kamanda Sirro akionesha vyeti bandia vya sekondari.
3.Nyaraka na vyeti mbalimbali vilivyokamatwa na jeshi la polisi jijini Dar es Salaam.
Nyaraka na vyeti mbalimbali vilivyokamatwa na jeshi la polisi jijini Dar es Salaam.
2.Baadhi ya vyeti Bandia vya Mamlaka ya Mapata TRA vilivyokamatwa.
Baadhi ya vyeti Bandia  vya Mamlaka ya Mapato (TRA) vilivyokamatwa.
JESHI la polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limekamata mitambo na vyeti mbalimbali vya shule za msingi, kuzaliwa, sekondari, biashara, stika za magari za TRA, bunduki moja na bastola maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam ikiwemo eneo la Pugu.
Akizungumza na wandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro amesema kuwa vyeti hivyo na mitambo ya kuchapisha ilikamatwa katika oparesheni maalum iliyofanyika Julai mwaka huu, huku taarifa zingine zikitolewa na wananchi kukabiliana na waharifu hao.
Amesema majambazi waliokamatwa bado majina yao yanahifadhiwa kwa ajili ya uchunguzi zaidi na watuhumiwa wa vyeti bandia bado wanaendelea kuhojiwa na uchunguzi ukikamilika watafikishwa mahakamani.
Kamishna Sirro amewataka wale wote wanaotumia vyeti bandia kujisalimisha kabla ya oparesheni kali itakayowachukulia hatua kuanza kwani inaonesha watuhumiwa baada ya kubanwa waliwataja baadhi ya vigogo waliotengenezewa vyeti hivyo na kuajiriwa serikalini na taasisi zingine

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA