SSRA yazungumzia hofu ya wananchi kuhusu mifuko ya hifadhi ya jamii
Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Onorius Njole (kushoto), akitoa ufafanuzi mbalimbali kwenye semina ya siku moja ya wanahabari kuhusu mifuko ya jamii Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Uhamasishaji, SSRA, Sarah Kibonde. Na Dotto Mwaibale MAMLAKA ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii nchini (SSRA), imewataka Watanzania kuondoa hofu iliyojengeka kwenye jamii kuwa mifuko ya hifadhi ya jamii ina hali mbaya kifedha. Akizungumza katika warsha maalum ya siku moja ya waandishi wa habari, iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa SSRA, Ansgar Mushi alisema kuwa mifuko hiyo haina hali mbaya kama wanavyodhani watu katika jamii kwani ina fedha za kutosha. “Watanzania wamekuwa wakiambizana kuwa mifuko hii ina hali mbaya kifedha, napenda kuwahakikishia kuwa ina fedha za kutosha kwani tumekuwa tukifanya ukaguzi wa mara kwa mara. Katika kaguzi zetu za m