SEMINA YA KAMATA FURSA TWENDEZETU KWA VIJANA YAFANYIKA LEO JIJINI MWANZA
Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Mh Stephen Masele akizungumza mada iliyohusu fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye nishati na madini ndani ya semina ya kamata fursa twendzetu,iliyofanyika mapema leo ndani ya ukumbi wa Gold Crest. Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Mh Stephen Masele akimtambulisha mmiliki wa hotel kubwa ya kitalii hapa jijini Mwanza, Gold Crest,Bwa.Mathias Erasto,ambaye pia ni mchimbaji mdogo wa madini,aliyajipatia fursa mbalimbali na kuzitumia ipasavyo na kufikia hapo alipo kimafanikio. Mkuu wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida,Mh.Yahaya Nawanda akizungumzia mada yake iliyohusu suala la ufugaji,hasa kuku wilayani mwake,ambapo pia amewataka vijana kuitumia fursa ya ufugaji wa aina yoyote katika suala zima la kujiletea maendeleo kwa namna moja ama nyingine badala ya kusubiri Serikali iwafanyie ama iwaletee kila kitu hapo walipo. Naibu Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia,Mh Januari Makamba akizungumza...