SEMINA YA KAMATA FURSA TWENDEZETU KWA VIJANA YAFANYIKA LEO JIJINI MWANZA
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini,Mh Stephen Masele akizungumza mada
iliyohusu fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye nishati na madini ndani
ya semina ya kamata fursa twendzetu,iliyofanyika mapema leo ndani ya
ukumbi wa Gold Crest.
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini,Mh Stephen Masele akimtambulisha mmiliki wa
hotel kubwa ya kitalii hapa jijini Mwanza, Gold Crest,Bwa.Mathias
Erasto,ambaye pia ni mchimbaji mdogo wa madini,aliyajipatia fursa
mbalimbali na kuzitumia ipasavyo na kufikia hapo alipo kimafanikio.
Mkuu wa
Wilaya ya Iramba mkoani Singida,Mh.Yahaya Nawanda akizungumzia mada yake
iliyohusu suala la ufugaji,hasa kuku wilayani mwake,ambapo pia
amewataka vijana kuitumia fursa ya ufugaji wa aina yoyote katika suala
zima la kujiletea maendeleo kwa namna moja ama nyingine badala ya
kusubiri Serikali iwafanyie ama iwaletee kila kitu hapo walipo.
Naibu
Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia,Mh Januari Makamba
akizungumza kwenye mada yake iliyohusu masuala mbalimbali, kuhusiana na
Fursa ya kuongeza thamani na kutengeneza jina,sambamba na fursa ya
matumizi ya Teknolojia mbele ya maelfu ya vijana waliojitokeza kwa wingi
mapema leo kwenye semina ya kamata fursa twendzzetu,iliyofanyika leo,ndani ya ukumbi Gold Crest,jijini Mwanza.
Sehemu
ya wakazi wa mji wa Mwanza waliojitokeza kwa wingi mapema leo kwenye
semina ya kamata fursa twendzetu,wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri
ukumbini humo,ambapo mada mbalimbali zilikuwa zikizungumzwa.
Mmoja wa wasanii wa bongofleva,Nikki Wa Pili akizungumza kwenye semina ya kamata fursa twendzetu.
Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya Maxcom inayouza bidhaa yake ijulikanayo kama Max
Malipo,Bwa.Juma Rajab akizungumzia kuhusiana na fursa ya bidhaa yake ya
Max Malipo inavyoweza kuisadia jamii kwa namna moja ama nyingine.
Baadhi Washiriki wakifuatilia.
Mmoja
wa waigizaji mahiri wa filamu hapa nchini Elizabeth Michael akijulikana
zaidi kwa la kisanii kama Lulu akiwasili kwenye semina ya kamata fursa
Twendzetu,ndani ya ukumbi Gold Crest,jijini Mwanza asubuhi hii,ambapo
pia atazungumzia mambo kadhaa mbalimbali kwenye semina hiyo,ambayo
itawakutanisha Naibu Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia,Mh
Januari Makamba,Mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini na watoa mada
wengine mbalimbali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB),Bi.Magreth Chacha alipokuwa akiwasili kwenye semina ya kamata fursa Twendzetu,ndani ya ukumbi Gold Crest,jijini Mwanza asubuhi hii.
Naibu Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia,Mh Januari Makamba akiwa ameambatana na Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Mh Stephen Masele (mwenye miwani) akisalimiana na Mkurugenzi wa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB),Bi.Magreth Chacha walipokuwa wakiwasili kwenye semina ya kamata fursa Twendzetu,ndani ya ukumbi Gold Crest,jijini Mwanza asubuhi hii,pichani kati ni Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji Clouds Media Group,Bwa.Ruge Mutahaba.
Baadhi ya Wakazi wa mji wa Mwanza na vitongoji vyake wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwenye semina ya kamata fursa Twendzetu,ndani ya ukumbi Gold Crest,jijini Mwanza asubuhi hii.

Comments
Post a Comment