KAULI YA MEMBE BAADA YA RAIS MAGUFULI KUFUTA SAFARI ZA WATENDAJI WA SERIKALI
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amempongeza Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli kwa kupiga marufuku safari za nje ya nchi, akisema mawaziri na watendaji wa Serikali walikuwa wakigongana angani na ndege utadhani Tanzania ilikuwa ikiwaka moto. Mbunge huyo wa zamani wa Mtama alisema uamuzi huo utaokoa fedha nyingi za Serikali na kumtaka Rais kushusha rungu hilo hadi kwenye mashirika. Wakati Membe akieleza hayo, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue alisema kila safari ya nje ina gharama yake na kila safari itakayofutwa zitapatikana fedha kusaidia masuala mengine ya maendeleo katika jamii. Juzi, Dk Magufuli alipiga marufuku safari za nje ya nchi kwa watendaji na kwamba shughuli ambazo wangekwenda kuzifanya, kuanzia sasa zitahitaji kibali kutoka kwake au zitafanywa na mabalozi wa Tanzania walioko katika nchi husika. Jana Membe alisema: "...Tulikuwa tunagongana huko hewani utadhani huku nyumban...