MAMBA KULINDA WAFUNGWA HATARI INDONESIA
Indonesia huwa na sheria kali sana za kukabiliana na
walanguzi wa mihadarati
Mkuu wa shirika la kupambana na dawa za kulevya Indonesia
amependekeza mamba watumiwe kulinda wafungwa waliohukumiwa kunyongwa.
Budi Waseso anataka taifa hilo lijenge gereza kwenye
kisiwa na kizingirwe na mamba akisema wanyama hao ni walinzi bora kushinda
wanadamu, kwani hawawezi kuhongwa.
Amesema atazuru maeneo mbalimbali katika taifa hilo
kutafuta mamba wakali zaidi.
Indonesia ina moja ya sheria kali zaidi za kupambana na
dawa za kulevya duniani na ilianza tena kunyonga watu baada ya kusitisha hukumu
hiyo kwa miaka mine 2013.
"Tutaweka mamba wengi sana huko,” Bw Waseso
alinukuliwa na tovuti moja nchini humo kwa jina Tempo.
"Huwezi kuwahonga mamba. Huwezi kuwashawishi
waruhusu washukiwa watoroke.”
Mpango huu bado umo katika hatua za mwanzo mwanzo nab ado
haijaamuliwa gereza hilo litakuwa wapi na ni lini litafunguliwa, shirika la
habari la AFP limesema.
Comments
Post a Comment